Napingana na wanaosema Afya ya Rais si siri

Kufikia hapa, unapiga propaganda tu hakuna lolote linalohusiana na kichwa cha mada yako; kwa hiyo tayari umekwishaififisha mada yenyewe.

Basi ngoja nijibu kichwa cha mada, maanake nimechoka kupoteza muda kusoma hadi huko chini.

"Napingana na wanaosema afya ya rais si siri"

Ikiwa ni siri watu watajua kuwa huyo rais hawezi kuumwa?

Wewe umejuaje kuwa hayo uliyobuni ndiyo sababu rais haonekani hadharani!
 
Suala la afya ya Mh. Rais yajadiliwa kwa mapana huku yakiangaliwa pia masuala kadhaa mtambuka

 
Kama ni siri zile pushap zilikuwa kutuonesha nini ama alikuwa anajifurahisha?
Zile pushups alifanya kwenye Jukwaa la Mkutano wa hadhara wa kampeini kuonyesha yuko imara baada ya minong'ono ya hali ya Afya yake kuzagaa mitaani na alishinda Uchaguzi na kuongoza nchi miaka 5 bila tatizo lolote la kiafya. Katika Uongozi wake alijiwekea utaratibu wa kujionyesha kwa kila alichofanya au alichosema ili asifiwe na kupongezwa mpaka wakati mwingine tabia hii ikawa inawakera watu na kuwafurahisha wengine. Pale Ikulu shughuli ndogo tu ikifanyika, makamera yote ya Luninga yatakuwa pale kuujulisha ulimwengu kinachoendelea na viongozi wa Chama, Mashekhe, Maaskofu, Wakuu wa Vyombo vya Usalama, uongozi wa Bunge, Mahakama nk watakaribishwa kushuhudia. Wasiwasi ulianza kujitokeza siku Mabalozi 3 wa Nchi za Nje walipokuja kwa mara ya kwanza kuwasilisha Hati zao Utambulisho ili waanze kazi Tanzania, badala ya kupokelewa na Rais Ikulu kama ilivyo kawaida, walipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje bila mbwembwe zilizozoeleka. Huko nyuma tumeona Rais anakwenda Kivukoni kununua samaki au ananunua mahindi ya kuchoma au kununua jogoo au kule Ikulu Chamwino tumeona anajianika kwenye mawe kama mjusi kwa dunia yote kumwona. Kama hayupo Ikulu ya Dar atakuwa Ikulu ya Dodoma au Chato na wananchi watajua alipo maana misafara yake ya kuelekea huko haijawahi kuonekana toka tupate Uhuru na kabla. Wananchi kuulizia Kiongozi wao kama mgonjwa si kosa kabisa ila kusema mgonjwa anaugua ugonjwa fulani ni kosa kwa sababu hata mgonjwa mwenyewe anaweza asijue anaugua nini mpaka aambiwe na Daktari baada ya kumpima. Tatizo kuna magonjwa yanajulikana bila Daktari!
 
Wanotaka Rais ajitokeze ndio wale juzi walikuwa wanasema anazurura sana wakati kuna Corona, ila binadamu sio.

Mimi namshauri mzee watu aendelee kuzingatia ratiba yake
Azingatie katiba yake na malaika
 
😂😂 SI KWELI. Labda ingekuwa suku 2, 3 au 4. Lakini how come sasa iwe karibu mwezi sasa Jiwe halionekani...??

Unasema anapitia mafaili ya nini eti?

Ya marehemu KM Balozi Kijazi...?

Kwani yeye Magufuli alisafiri safari ndefu ya mwezini na kumkuta KM wake Kijazi kafariki na sasa amerudi na anataka kujua kuna nini ktk mafaili hayo...??

Inafurahisha sana. Maana wengine wanasema eti yuko chimbo anapitia jina la Katibu Mkuu wa CCM kisha ateue...

Huyu huyu arrogant & boastful Magufuli asiwe kwenye Spotlights kwa karibu mwezi sasa?

ABSOLUTELY, IMPOSSIBLE. JIWE ANA SHIDA, ANA TATIZO SI BURE....!;
 
wacha nikugeuzie kifuu, kama wewe una ushahidi kwamba haumwi weka wazi hapa, na sio ushahidi wa fulani kasema.
Taifa lina haki kabisa kuuliza alipo rais wao pale anapotokea kutoonekana kupita desturi yake. Wewe mwenyewe unakumbuka ni lini toka jiwe awe madarakani kushindwa kurushwa hutuba zake za kanisani kila jumapili? Hilo halikufanyi kujiuuliza ni kwa nini ghafla asionekane? Hushangai ni kwa nini ameshindwa kuhudhuria mkutano wa viongozi wa EAC ambao ulikuwa virtual? Kwa nini awe popote pale alipo alishindwa kuhudhuria? Yote hayo bado bichwa lako linakubali kudanganywa tu?
 
Safi sana mleta mada...Katiba inasema pia Rais anayo mamlaka ya kukataza vyama vya Upinzani kufanya siasa ila ni Chama chake tu kinacho ruhusiwa kufanya Siasa wakati wote na sehem yoyote
 
Unaongea kama mtoto, uliwahi kuona wapi kiongozi wa nchi akifanya kazi hivyo.

It's just a matter of time before we know the truth something that will be a setback to the government.
 
Safi sana mleta mada...Katiba inasema pia Rais anayo mamlaka ya kukataza vyama vya Upinzani kufanya siasa ila ni Chama chake tu kinacho ruhusiwa kufanya Siasa wakati wote na sehem yoyote
Atupe kifungu cha katiba kinachompa hayo mamlaka.
 
Bila kutetea upande wowote. Unfortunately, once a Public figure you cease having a private life - your life is for public consumption and scrutiny. Ndio maana wengine hawajaingia kuwa viongozi wa dini, siasa, royal family n.k kwa sababu hii. Waulize hata wale wanaojiita Emir wa ISIS.

Kwa kila choice we make - there are sacrifices.
 
Yaani mitandaoni huku wamejaa wahuni watupu mtu anakaa anaamua kuanzisha uzushi kisa ameshiba kande zake.
 
Nchini kuna vyombo zaidi ya 90% vinamilikiwa binafsi, na pia kuna vyombo vya habari vya mataifa ya nje, na Balozi mbalimbali. Hivi, inaingia akilini upana huo wa kupata na kutoa habari umeshindwa bali tutumie mitandao ya kijamii! JIFIKIRISHE
 
Weka orodha ya mwonekano wa Rais hadharani ili hoja yako iwe na uzito.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…