Kizito Dickson
Senior Member
- Sep 24, 2018
- 174
- 209
Huyu bwana alikuwa emperor,mfalme wa dola ya ufaransa katika miaka ya 1800.
Alikuwa ni mmoja kati ya mashuja wa kipekee waliowahi kutokea katika historia ya ufaransa.Baada ya mapinduzi ya ufaransa,Napoleone aliibuka na kuwa mmoja kati ya majemadari bora kabisa wa Jeshi la ufaransa.
Aliongoza mapambono ya kutuliza ghasia ndani ya ufaransa hasa na baadaye akajitangaza mwenyewe kuwa Mfalme.
Baada ya kuwa mfalme alianza vita za kutaka kuteka na kutawala ulaya ambapo baada ya miaka 6 ya vita alishindwa na kupelekwa kizuizini katika kisiwa kidogo katika bahari ya mediteranean na Mdogo wa Mfalme wa ufaransa aliyevuliwa madaraka akachukua kiti chake.
Huyu bwana aliwahi kuja mpaka Afrika huko Misri kwa lengo la kutaka kuwazuia waingereza kufanya biashara.
Hata hivyo pamoja na kufungiwa katika kisiwa hicho baada ya miezi michache alitoroka na kurudi ufaransa na kisha kuteka himaya yake kwa mara ya pili.Aliingia katika vita dhidi ya urusi ambapo TZAR Alexander wa Urusi aliona bora achome mji wake mkuu kuliko kuruhusu Napoleone auteke na kuutumia
Alishindwa vibaya katika mapambano yaliyotokea huko Waterloo Ubelgiji ambapo alipigwa hadi kukimbia na kikosi cha kamanda wa majeshi ya uingereza
Huyu ni mmoja kati ya mashuja wa kihistoria mbao tunapaswa kuwafahamu kama ambavyo tungependa kuwafahamu mashujaa wengine wa historia ya Afrika na dunia