Naporwa Nyumba kwa Sababu ya Mkopo wa 3rd Part

Naporwa Nyumba kwa Sababu ya Mkopo wa 3rd Part

sangas

Senior Member
Joined
Aug 26, 2012
Posts
135
Reaction score
95
Ndugu wanasheria niwekeni sawa kwa hili,

Kampuni yetu ina nyumba mjini, na mmoja wa wanahisa alikopa katika taasisi fulani na akaweka hati ya kampuni (bila makubaliano).

sasa mkopo hakumalizika kulipwa na wameshauza nyumba,nilifungua kesi, mhisa hakutokea naomba ushauri nifanyeje?
 
hakutokea mahakamani kwa kuumwa hakimu akaondoa kinga ya kimahakama na nyumba siku ya pili ikauzwa.sasa naomba msaada nifanye nn kuweza kupata nyumba tena ili ibaki mikononi mwa kampuni, nikate rufaa na nyumba imeshauzwa
 
Ili hati ya nyumba inayomilikiwa na kampuni iwe dhamana kwenye mkopo wa taasisi za fedha ni lazima mambo haya yafuatayo yafanyike.

1. Lazima kuwe na madhimio ya kikao cha kampuni kuruhusu hati hiyo kuwekwa kama dhamana (board resolution)

2. Lazima kuwe directors guarantee.

Sasa sijui huyo bwana alifanikiwaje kuweka hati hiyo kama dhamana bila kuwashirikisha nyie ma director wengine wewe ndio utuambie sababu naamini benki pia haiwezi kumkubalia bila idhini yenu.
 
hakutokea mahakamani kwa kuumwa hakimu akaondoa kinga ya kimahakama na nyumba siku ya pili ikauzwa.sasa naomba msaada nifanye nn kuweza kupata nyumba tena ili ibaki mikononi mwa kampuni, nikate rufaa na nyumba imeshauzwa

Kabra ya kukata rufaa tafuta wakili umweleze hayo yote umpe na vielelezo vyote ili aone kama there is a good case on your side.
 
Hapa nashindwa kuelewa.....Kwa sababu maamuzi ya Kampuni yanafanywa na shareholders wenye majority share....kwa kusaini kama signatories!
Pia huthibitishwa na mwanasheria wa Kampuni....sasa nashindwa kuelewa hiyo benki ilifanyaje bila taratibu zote za Legal person kufuatwa.
 
ulishindwa hata kuweka pingamizi la kuzuia maamuzi kuendelea mpaka kupata muafaka? mbona iko wazi.
 
hayo mambo tumeshakumbana nayo unapashwa kukata rufaa kabla ya siku 14 kama hukuridhia kwa wao kuuza nyumba wao wanasheria zao zinazo walinda ikiwa hukutimiza asilimia flani ya mkopo ndani ya robo tatu ya miaka ya marejesho wanapiga mnada fasta tena kwa bei ya hasara kama ni nyumba huuzwa kwa asilimia 25 ya tathmin ya serkali,jaribu kuonana na wanasheria pengine wanaweza kukupa msaada ukuhitaji lawyer ni pm
 
Back
Top Bottom