Nimekuwa na kawaida ya kutembelea vijiji mbali mbali, juzi nilikuwa Mufindi, nikakutana na Wachina kijijini Mapanda wanatafuta miti kwa ajili ya fenicha kiwandani kwao.
Siku moja nilikuwa kijijini kwetu, nikiwa kijiweni na madogo, nikashangaa kuona utitiri wa pikipiki, madogo wakaniambia hapa kuna pikipiki kama arobaini hivi.
Siku moja nilikuwa kijijini Kibengu, nikaona mtu anashusha sembe toka Mafinga,yaani unga utoke mjini uende kijijini, hali hii inaashiria nini? Nimepita juzi tena nikakuta nguzo za Rea zinasambazwa.
Nikafunguka macho, kwanini Wachina wale walikuwa wanapiga picha nyingi,halafu mimi wananidanganya kwamba wanatafuta miti ya mbao wakati miti iko Mafinga. Nikaona kumbe boda boda zile ni kiashiria cha mafuta kutumika sana na hivyo naweza kufungua kituo cha mafuta.
Lile sembe la Kibengu likanikumbusha, kuwa dunia inabadilika kwa kasi sana,naweza kusaga sembe kule kule kijijini na kuisambaza kule kule vijijini.
Wale Wachina niliowaona wanazuga kule Mapanda sio muda mrefu watatuliza,sio muda mrefu watafungua viwanda vidogo vidogo vijijini, kama una mtaji kidogo, hama mjini kawekeze kijijini, maana sio muda mrefu umeme ambao ndio moja ya nyenzo mhimu ktk uzalishaji utakuwa bwelele.