NASA ARTEMIS: Project ya kumpeleka binadamu katika mwezi

NASA ARTEMIS: Project ya kumpeleka binadamu katika mwezi

mike2k

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2016
Posts
1,571
Reaction score
3,448
Artemis program ni programu ya anga za mbali ambayo inakwenda kufanyia uchunguzi mwezi 🌒.

Program hii inaongozwa na NASA wakishirikiana kwa ukaribu kabisa na mashirika ya tafiti za anga kutoka nchi mbalimbali duniani Africa tukiwakilishwa na South Africa. Artemis program pia inazishirikisha kampuni binafsi zinazojishughulisha na space exploration kama Blue moon ya Bwana Jeff Bezos, Space X ya Elon Musk, Toyota, moon express, Airbus na kampuni nyingine nyingi.

Artemis program ilianza rasmi mwaka 2017 kama sehemu ya mpango wa US space exploration programme.
Ukiwa na malengo ya muda mfupi
Kumpeleka mwanamke angani na kumpeleka mtu mweusi katika space.

Malengo ya kati yakiwa ni kuanzisha ustawi wa shughuli katika mwezi katika kufanya tafiti mbalimbali katika mwezi.

Malengo makuu ya muda mrefu yakiwa ni kuweza kukusanya rasilimali mbalimbali zinazopatikanaa katika mwezi Lunar resources - Wikipedia

Na pia Artemis programme itasaidia kujenga msingi katika kuwezesha binadamu kufika katika sayari ya mars.

Nchi mbalimbali zinaalikwa kujiunga na Artemis programme kupitia ARTEMIS ACCORD Artemis Accords - Wikipedia

OVERVIEW
Artemis programme itahusisha kitu kinaitwa SPACE LAUNCH SYSTEM (SLS) MISSIONS. HUU NI mfululizo wa missions zitakazokuwa zinafanyika kwa awamu na zimepewa jina la Artemis 1, Artemis 2 ...........Artemis 5. Missions hizi zitakuwa na majukumu tofauti tofauti.

Artemis 1
mission itafanyika tarehe 29 agoust 2022.



ARTEMIS 1 (2022) itakuwa ndo phase one ya programme hii ikiwa ni sehemu ya majaribio kwa SLS launcher na Orion spacecraft.​

Katika majaribio haya NASA and hers partners wanategemea kuituma hii orion 🌌 🚀 spacecraft katika orbit ya mwezi na kisha baada ya siku sita kuirudisha tena duniani.

N.B
HII Mission unaweza kuifatilia kwa ukaribu zaidi kupitia mitandao yao ya kijamii

Mtambo upo tayari kwa ajili ya kuanza safari tarehe 29 August 2022
1658655975410.jpg

Katika mfululizo wa makala hii tutakuwa tunaeleza kinagaubaga MISSIONS ZOTE.

Kama una swali lolote kuhusu moon mission karibu hapa tujifunze.
 
Nipo nimekaa hapa nafuatilia.
 
Back
Top Bottom