NASA wapanga kuanza maandamano ya kutoitambua serikali wiki ijayo

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Muungano wa NASA sasa umeashiria kuwa wafuasi wake watarejelea maandamano wiki ijayo. Mikutano ya viongozi wa NASA leo, imepanga mikakati ya maandamano hayo ambayo yanadhamiria kuonyesha kutoitambua serikali.

Kadhalika NASA inapanga orodha ya bidhaa na huduma zitakazosusiwa na wafuasi wake ikiwa ni pamoja na majengo ya kibiashara ambayo imetundika picha ya Rais Kenyatta. Viongozi wa Jubilee wanamtaka kinara wa nasa Raila Odinga kulegeza msimamo kulisaidia taifa kusonga mbele.

Wamesema maandamano hayo yatakuwa ya amani na wametoa mafunzo kwa watu watakaoyaongoza ili yasidhuru wananchi wengine

 
hiyo nchi bana watajijua wenyewe
 
Hot air demonstrations yielding nothing except for fatigue and more disappointments.
 
hawa viongozi wakae wakubaliane, kwa mustakabali na maslahi mapana ya nchi yao.
 
wametoa mafunzo...aisee yangu macho maana wenye kuadamana hudai bila kukimbizana na polisi maandamano hayanogi
 
Wajinga na wanafik wa NASA waache ujinga huu. Uchumi imeporomoka 1% na pesa meli mzima zimetumika kwa uchaguzi,wawekezaji wametoweka na biashara imepungua.

Nonsense tumechoka na uchaguzi usiyo na mwisho watu warudi kazi .Kenya doesn't revolve around Odinga and his selfish quest for office.
 
Waafrika tuna matatizo kibao ya kuyashughlikia ila hizi siasa ndiyo tumeziweka mbele kuliko jambo lengine lelote.
 
Huyu jamaa kumbe m binafsi sana sizani kama angekuwa chaguo sahihi coz analazimisha watu wafate anayotaka yeye kweli dunia ya Leo hii mbinu haitumiki tena amechemka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…