NASA yasisitiza hakuna uchaguzi utaandaliwa bila matakwa yao kutimizwa

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Muungano wa NASA unasisitiza kwamba hakuna uchaguzi utaandaliwa tarehe 17 mwezi Oktoba ikiwa matakwa yao hayatatimizwa. Wakiwahutubia wanahabari, viongozi wa NASA hata hivyo walipuuzilia mbali habari kwamba watasusia marudio ya uchaguzi wa urais, wakisema hakuna uchaguzi utaandaliwa ikiwa rufaa waliowasilisha kwa tume ya uchaguzi jana haitashughulikiwa. Kinara mwenza wa muungano wa NASA ambaye pia ni seneta wa Bungoma Moses Wetangula alisema walikabidhi tume ya uchaguzi rufaa hiyo wakiorodhesha matakwa yao ya kufanywa uchaguzi wa kuaminika. Alisema miongoni mwa matakwa hayo ni kufutwa kazi kwa afisa mkuu wa tume ya IEBC, Ezra Chiloba, kushtakiwa kwa baadhi ya wafanyikazi wa vyeo ya juu wa tume hiyo na kuchunguzwa kwa server za tume hiyo. Aidha Wetangula alisema upinzani hautajiunga na kamati yoyote ya bunge kwani bunge limeundwa kinyume cha sheria. Alisema watawafungulia mashtaka ya kibinafsi maafisa wa tume ya IEBC watakaopatikana na hatia ya kuvuruga uchaguzi mkuu tarehe nane mwezi Agosti. Upinzani uliwahutubia wanahabari jana baada ya mkutano wa kundi la wabunge wa NASA katika makao makuu ya Okoa Kenya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…