Pre GE2025 Nasaha kwa Chama changu cha Mapinduzi (CCM)

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Wolle Melkas Fernando

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2016
Posts
253
Reaction score
360
Kufuatia kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh. Ndugu Tundu Lissu ya '𝑡𝒐 π‘Ήπ’†π’‡π’π’“π’Ž, 𝑡𝒐 π‘¬π’π’†π’„π’•π’Šπ’π’' kumekuwa na 'reactions' nyingi kutoka kwa viongozi mbalimbali, matawi na taasisi mbalimbali za CCM wote wakijibu Kauli ya 'No Reform No Election.'

Kutokana na kinachoendelea, Kuna machache ya kuchangia ili kuokoa Chama na kujenga amani ya nchi.

Kwanza; Wanaccm wote lazima tufahamu kuwa Kumjibu Mh. Tundu Lissu hakuhitaji mihemko na kejeli Bali ni kutumia akili, tukitumia mihemko na kukurupuka
tutacheza Kila ngoma itakayopigwa na Tundu Lissu.

Kwa Muktadha huu, jambo la muhimu ccm ilipaswa kuwa na mtu mmoja ama msemaji mmoja ambaye angekuwa anashirikiana na idara yake ya usemaji kujibu kwa akili Kauli na misimamo ya Chadema.

Vilevile haipaswi kuwa na Kauli za Kila mtu Kumjibu Lissu, kiasi kwamba hata Chipukizi wanaamua tu kutoka na Kauli ya Kumjibu Lissu.

CCM tuna Faida kubwa sana, kwanza ni Chama Kikongwe chenye wananchama wengi na historia kubwa, suala la kupigiwa ngoma na Chadema na wote kuicheza, inaonesha hatujiamini. CCM Kama Chama tawala na miongoni mwa vyama vikubwa Afrika tulipaswa

1. Badala ya kukurupuka, CCM ingekuwa bora kujibu kauli ya Lissu kwa kuelezea wazi jinsi ambavyo tunatambua changamoto za kisiasa zinazoikumba nchi Yetu na kuonyesha wazi msimamo wetu kuhusu mchakato wa mageuzi ya kisiasa. Ingekuwa vizuri ikiwa CCM ingesema wazi kuwa inakusudia kwa dhamiri safi ya mageuzi yenye manufaa kwa ustawi wa demokrasia, lakini huku ikisisitiza kwamba mageuzi hayo yatekelezwe kwa njia ya kikatiba na katika misingi ya utawala wa sheria hapa tungekuwa tunaoneaha ukomavu na kwamba hatuogopi Reform s zozote za uchaguzi Huru na Haki.

2. Zaidi ya hayo, CCM tungekuwa na manufaa zaidi ikiwa tungeonesha kuwa tunashirikiana na wadau mbalimbali katika mchakato wa mageuzi, ikiwa ni pamoja na Upinzani wenyewe, ili kuhakikisha kuwa uchaguzi ujao unakuwa wa haki na uwazi. Kujibu kwa busara na kwa kuzingatia maslahi ya taifa kungeweza kusaidia kulifanya taifa kutokuwapo kwenye mivutano isiyo ya lazima lakini kubwa kabisa Kukiweka Chama Cha Mapinduzi Katika Hali ya Kujiamini na Salama zaidi kuliko kejeli.

3. CCM tungekuwa na manufaa zaidi ikiwa tungeonyesha kuwa tunashirikiana na wadau mbalimbali katika mchakato wa mageuzi, ikiwa ni pamoja na Upinzani wenyewe kuweka mambo sawa, ili kuhakikisha kuwa uchaguzi ujao unakuwa Huru na wa Haki na Uwazi. Kujibu kwa busara na kwa kuzingatia maslahi ya taifa kungeweza kusaidia kulifanya taifa kutokuwapo kwenye mivutano isiyo ya lazima na zaidi sana kuihakikishia CCM kuwa mahali salama zaidi kuliko kutumia vitisho na mabezo.

4. Kumjibu Lissu kama nilivyosema awali hakuhitaji mihemko wala kejeli, tulipaswa kuisisitiza CHADEMA kuwa pamoja na hitaji la Mageuzi lakini tunahitaji umoja na mshikamano wa kitaifa kujadili pamoja ili kulinda Tunu ya amani ya nchi Yetu, nadhani kwa uelewa wangu haya yangekuwa ni majibu bora zaidi. Badala ya kujibu kwa hisia, kejeli au kushambuliana, CCM ingekuwa na manufaa ikiwa ingeonyesha kuwa inahitaji ushirikiano wa pande zote za kisiasa na jamii kwa ujumla, ili kuhakikisha nchi inasonga mbele kama taifa lenye utulivu na amani.

Kuliwahi kutokea tuhuma za upotevu wa Trilioni moja Serikalini, kilichofanyika ni kwamba hakukuwa na Kauli moja Madhubuti ya Chama iliyonyook na yenye majibu ya kushiba kama Chama tawala, badala yake Kila taasisi ya CCM ilijitokeza kujibu kwa kejeli mapigo ikiwemo UWT, UVCCM, Jumuiya ya Wazazi, Chipukizi n.k. Hii ni Hatari sana kwa ustawi wa Chama au taasisi yoyote kwasababu hakukuwa na majibu ya kufanana.

Na Kama CCM hatutajirekebisha kwa hili basi tutarajie kucheza mapigo ya ngoma ya aina yoyote kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Kikuu Cha Upinzani Ndg. Tundu Lissu.

Yote kwa Yote, Tanzania ni Moja na Lengo ni Moja, Kufuta Umaskini, Kuleta Maendeleo ili Watanzania waishi Maisha Bora Zaidi. Tusigombanie Fito wakati tunajenga Nyumba Moja.
 
Maneno kuntu kabisa lakini tegemea kupingwa kwa kejeli bila kujibu hoja toka kwa chawa wa kijani.
 
Kauli ya lissu ni kauli ya kizalendo kabisa! Lakini machawa wa CCM wao kila jambo likizugumzwa na mpinzani linaonekana halina maana! Ni upumbavu wa hali ya juu! Sana!
 
Nimeipenda hii comrade
 
Back
Top Bottom