ToniXrated
JF-Expert Member
- Sep 21, 2022
- 1,134
- 2,993
Amani iwe nanyi.
Natumaini wachezaji na viongozi wangu wa chama langu la Wekundu wa Msimbazi wapo salama kabisa.
Bila ya kupepesa macho wala kung'ata maneno napenda niwaase wachezaji kuwa waingie uwanjani huku wakiwaheshimu wapinzani wetu De Agosto, wakumbuke kuwa haijaisha mpaka iishe.
Jana tumeshuhudia jinsi timu za Wanaija zilivyong'olewa katika Klabu Bingwa na Shirikisho licha ya kuibuka na ushindi mzuri katika mechi za mkondo wa kwanza. Kwara United na Rivers United zote nje huku Plateau United naye akifuatia.
Wanaija walifurahia kuwafunga Waarabu nyumbani kwao ila hawakuamini macho yao walipocheza mechi hizi za mkondo wa pili. Hivyo naiomba sana timu yangu ya Simba kuwa makini na kuwaheshimu wapinzani wetu ili tujihakikishie kutinga hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika kwa mara nyingine tena.