Nasema kweli

Nasema kweli

PSPA Pure'12 udsm

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2013
Posts
832
Reaction score
447
Watanzania, Vijana wenzangu,wazazi, wadogo zangu,kaka zangu,dada zangu, tuache mizaha, tuache siasa, tuache kila kitu walau hata kwa sekunde tano,tujiulize nchi hii inakwenda wapi? tupo katika hali mbaya sana, ni wajibu wako, ni wajibu wangu kuleta mabadiliko.

Matokeo haya ya vijana wetu, kwa sasa unaweza ona kama hayakuhusu,lakini mwisho wa haya yote ni anguko kuu, kwa nini tusianze sasa,kwa nini tusiseme basi, kwa nini tuendelee kutengeneza vijana wasiojiweza kifikra kwa namna hii,kama tunashindwa kubadilisha na kusimamia mambo madogo ya namna hii, tutawezaje kusimamia yale yaliyo makubwa.

Kutokua na elimu bora kwa vijana ni cancer,inapoanza huwezi kusikia maumivu, lakini siku zote mwisho wa cancer ni kifo, Tunaweza kubadilisha mwanzo huu mbaya,kama wewe na mimi tutaona umuhimu wa kufanya hivyo naandika mambo haya kwa uchungu
sana, na najua No One cares. But if you read this, i want you to start caring.

kwa matokeo haya, na mengine mengi yanayotokea ndani ya nchi hii, na kwa level ya ufikiri na utendaji uliopo sasa, kama hatutachukua hatua,tutachelewa sana.

Mabadiliko ni wewe, ni mimi.
 
Back
Top Bottom