Nasema na wewe

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
Usiyejua maana ya upendo kutwa kucha unamfanya mwenzio kama kinanda anakulilia wewe na wala hujali thamani ya machozi yake. Siku zako zinahesabika ipo siku na wewe utalia zaidi yake.

NASEMA NA WEWE
Dada usijielewa kuwa wewe ni mke wa mtu, yaani mumeo akitoka nyumbani na wewe unatoka kiguu na njia kwa mashoga zako kwenda kuzungumza umbea wa mitandaoni mara diamond mara zari, Gigi money na wakina Hamisa mobeto, chunga sana ndoa yako ipo njiani kuvunjika hao watafuta kiki za mitandaoni hawatalitambua hilo, unaivunja ndoa yako kwa mikono yako.

NASEMA NA WEWE
Unaejiita mume wa mtu, kila siku wewe na mpira umekariri majina ya wachezaji kama kocha wa timu yako, huna muda na mkeo yaani ukitoka kwenye utafutaji wako wa ridhiki moja kwa moja kwenye magenge ya mpira. Jiandae kumuona mkeo akichepuka na mtu anyejua thamani ya muda kwenye mapenzi.

NASEMA NA WEWE.
Dada unayepoteza muda wako kujikita kwenye mahusiano na mume wa mtu, tambua kuwa kila lenye mwanzo halikosi mwisho, sasa wewe jiachie na mume wa mtu ukadhani utakuwa nae daima, la hasha, unachezewa bure mwisho wa siku anarudi kwa mkewe ila tambua machozi ya mwanamke mwenzio hayapotei bure, utaachiwa laana itakayodumu kwenye maisha yako yote hautapata mwanaume mwaminifu kamwe katika maisha yako.

NASEMA NA WEWE
Dada uliyekolea kwenye mapenzi yasiyo na ndoto wala tija na brother man, sharo baro, mlamba lips, mwenye kuvaa buti kubwa na jinsi ya kuchanika chanika, mnyoa viduku, mvaa vipuri, muda wote anatembea na self stick na mbaya zaidi anakaa kwao, nakupa pole sana dada angu huyo bado ni mtoto wanyumba hapo alipo hana mbele wala nyuma pesa ya kununua vocha ya kuongea na wewe tu hadi ampinge mzinga dady, alafu bado unajisifia unamchumba POLE SANA. kama anakupenda kwanini asikupeleke kwa wazazi wake. Kila anapokuhitaji unaishia lodge na nyumba za wageni akijitahidi saana labda aazime funguo ya geto kwa rafiki yake. Unapoteza muda dada angu kimbia kwa huyo mtoto

NASEMA NA WEWE
Mwanaume unayepachika mimba watoto wa watu alafu unakimbia au kuwatelekeza mabinti wa watu, hiyo damu unayoitupa haipotei bure. Tambua kulaghai mabinti na kuwatia mimba alafu unatoweka utambue yakwamba mungu anakuona. Hizo mimba unazokimbia au kuwashawishi mabinti wazitoe ujue zinaondoka na nguvu zako. Itakapofika kipindi unahitaji mtoto ndipo utagundua mimba haikataliwi. Jiandae dawa yako inachemka.

NISAIDIE KUSHARE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…