Nashauri Ajira za masaa kupunguza tatizo la ajira nchini

Nashauri Ajira za masaa kupunguza tatizo la ajira nchini

Aikasia James

Member
Joined
Jun 21, 2024
Posts
5
Reaction score
1
Shida kubwa ni ajira kwa vijana wa sasa lakini kuna uwezekano wa kazi za masaa kama ilivyokuwa hospitalini kwamba kuna daktari ataingia usiku na mwingine asubuhi.

Makampuni hapa Tanzania ni mengi kidogo lakini pale ambapo vijana watafanya kazi kwa masaa hata idadi ya wasioajiriwa itapungua.

Yamkini watu wanasema kuwa tunabidi tujiajiri wenyewe sawa si shida tujiajiri lakini nani atafanyakazi kwenye kampuni fulani au hata kwenye ofisi ya fulani kama sio sisi wenyewe.

Watu wanavosema si vibaya lakini kama taifa tunabidi kuangalia kwa jicho la pili suara la ajira kwa ajili yetu sisi sote.

Ndio ujasiliamali upo lakini sio wate wanaoweza kujikita kwene hilo swala lakini hili jambo la kazi ya masaa itawafanya hata wale ambao hawana uwezo wa kufanya ujasiliamali kupata hata kazi ya kufanya. Kuna muda tunakosa hata watu wabunifu wa kazi kwa sababu tumebana riziki zao.

Maana mtu masaa 12 yeye tu hicho hicho kiti lakini kama kungekuwa na mabalishano ya kazi labda kila baada ya masaa tano basi kila mtu atapata nafasi ya kufanya kazi.

Hii ni nchi yetu sote na fursa ni yetu sote hata katika maendeleo tusiachane nyuma. Maana kwa wengine elfu kumi ni hela ndogo sana lakini kwa wengine pia ni hela kubwa sana.

Kama ni nafasi ya kazi basi tugawane kwa masaa wote tufaidike. Hiki kitu tukikifanya hata kwa mwaka mmoja tuone mabadiliko yanayoleta ninauhakika yatakuwa makubwa sana.

Maana hata mikopo vijana waliopewa na serikali wanashindwa kulipa lakini hii fursa itakuwa ni faida kwa serikali na vijana pia kwa ujumla.

Nina imani hata hili litasaidia kujenga taifa hili zuri la TANZANIA
 
Kwani ajira zilizopo si zipo kwa masaa? kwa ziku masaa 8 ya kazi.
Na shift zipo hasahasa 2
Kwenye viwanda vipo hadi vyenye shift 3.

Suluhisho labda viwanda viwe vingi na sekta binafsi ziwe nyingi.
 
Nadhani umekosea uwasilishaji wako, ila ajira za masaa ni wazo zuri, ila hazipo ulivyozisemea, goa and study How UK works.
 
Back
Top Bottom