Nashauri Akili ze Brain apewe asilimia ya mauzo na si hela ya mkupuo kwenye wimbo wa Jugni x Mond

Nashauri Akili ze Brain apewe asilimia ya mauzo na si hela ya mkupuo kwenye wimbo wa Jugni x Mond

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,424
Reaction score
4,954
Diamond amechukua vionjo vya ngoma ya Akili ze Brain inayoitwa Regina, akaenda kuomba kushirikiana na nyota mkubwa India mwenye mashabiki mabilioni na sasa kwa kutumia ubunifu wa Akili ze Brain na ustaa Jugni huko kwenye digital platform pesa zinaingia kila sekunde na ni nyingi zaidi ya matundu ya neti.

Ushauri wangu kwa Akili ze Brain, usije kuwa umeingia mtego ambao WCB na Diamond wanafanya kwa wasanii wanaotumia vionjo vyao kama Saida Caroli itakula kwako. Wanachofanya, anakuambia tu juu juu kuwa nakupa tuseme mil. 10 au 15 nataka kutumia vionjo vyako, hakwambii kuwa ataenda kushirikisha msanii mkubwa na nyimbo itakuwa inauza mpaka unakufa unajikuta umeingia KANYABOYA.

Sasa wewe mwambia akupe asilimia fulani ya kila mauzo yanapofanyika, huu ndiyo wakati wako kutajirika.
 
Diamond amechukua vionjo vya ngoma ya akili ze Brain inayoitwa Regina, akaenda kuomba collabo na star mkubwa India mwenye washabiki mabilioni kutoka India na Sasa Kwa kutumia ubunifu wa akili ze Brain na ustaa Jugni huko kwenye digital platform pesa zinaingia kila sekunde na ni nyingi zaidi ya matundu ya Neti.

Ushauri wangu Kwa akili the brain, usije kuwa umeingia mtego ambao wcb na diamond wanafanya Kwa wasanii wanaotumia vionjo vyao kama Saida caroli itakula kwako, wanachofanyaga anakuambia tu juu juu kuwa nakupa let say mil 10 au 15 nataka kutumia vionjo vyao, akuambii kuwa ataenda kushirikisha msanii mkubwa na Nyimbo itakuwa inauza mpaka unakufa unajikuta umeingia KANYABOYA,

Sasa wewe mwambia akupe % flani ya kila mauzo yanapofanyika, huu ndo wakati wako kutajirika.
Mbona ilisemekana kuwa ule wimbo pia akili aliusample kutoka kwenye wimbo mwingine wa kihindi?
Ile mimi ngoma yake ninayoikubali zaidi ni bongo bangla
 
Diamond amechukua vionjo vya ngoma ya akili ze Brain inayoitwa Regina, akaenda kuomba collabo na star mkubwa India mwenye washabiki mabilioni kutoka India na Sasa Kwa kutumia ubunifu wa akili ze Brain na ustaa Jugni huko kwenye digital platform pesa zinaingia kila sekunde na ni nyingi zaidi ya matundu ya Neti.

Ushauri wangu Kwa akili the brain, usije kuwa umeingia mtego ambao wcb na diamond wanafanya Kwa wasanii wanaotumia vionjo vyao kama Saida caroli itakula kwako, wanachofanyaga anakuambia tu juu juu kuwa nakupa let say mil 10 au 15 nataka kutumia vionjo vyao, akuambii kuwa ataenda kushirikisha msanii mkubwa na Nyimbo itakuwa inauza mpaka unakufa unajikuta umeingia KANYABOYA,

Sasa wewe mwambia akupe % flani ya kila mauzo yanapofanyika, huu ndo wakati wako kutajirika.
Akili the brain hiyo nyimbo ya Regina nae kakopi kila kitu kuanzia melody mpaka biti, alichofanya yeye kuweka maneno ya kuswahili basi ila hamna creativity wala ubunifu wowote kutoka kwake so hastahili hata Senti.Anaye stahili ni yule muhindi aliye kopiwa na akili the brain.

Saida Karoli nyimbo zake hana haki nazo,zipo chini ya aliyekuwa meneja wake na yy ndiye aliye lipwa na WCB, Rayvanny nae alirudia nyimbo ya Siri nae akamlipa yule mzee mwenye nyimbo.

Mfano Utaubeba ya Harmo, Mr Blue kalipwa hela yake? Darasa nae kuna nyimbo alikopi vionjo vya nyimbo moja hivi ya zamani (jina limenitoka),ila sijui kama kawalipa wale wazee?
 
Kuna kitu hujakielewa vizuri mtoa mada, kuna kuclear sample na lawsuit ya kutumia sample bila idhini mmiliki.

Kuclear sample siyo gharama kubwa sana kwa sababu unapewa ruhusa na mmiliki ama kuingia makubaliano na (timu yenye hati miliki) ya kutumia sample katika kazi yako ya sanaa. Na katika makubaliano hayo unaweza kuruhusiwa kulipa mara moja ama mmiliki akawa anapokea royalties za mauzo ya wimbo kwa asilimia fulani.

Kwa hiyo ukipelekwa mahakamani most of times utalipa fidia ikiwemo na faini kwa kutumia sample bila idhini ya mmiliki.
 
Diamond amechukua vionjo vya ngoma ya Akili ze Brain inayoitwa Regina, akaenda kuomba kushirikiana na nyota mkubwa India mwenye mashabiki mabilioni na sasa kwa kutumia ubunifu wa Akili ze Brain na ustaa Jugni huko kwenye digital platform pesa zinaingia kila sekunde na ni nyingi zaidi ya matundu ya neti.

Ushauri wangu kwa Akili ze Brain, usije kuwa umeingia mtego ambao WCB na Diamond wanafanya kwa wasanii wanaotumia vionjo vyao kama Saida Caroli itakula kwako. Wanachofanya, anakuambia tu juu juu kuwa nakupa tuseme mil. 10 au 15 nataka kutumia vionjo vyako, hakwambii kuwa ataenda kushirikisha msanii mkubwa na nyimbo itakuwa inauza mpaka unakufa unajikuta umeingia KANYABOYA.

Sasa wewe mwambia akupe asilimia fulani ya kila mauzo yanapofanyika, huu ndiyo wakati wako kutajirika.
Ungemshauri kabla hajakubali vionjo vya wimbo wake kutumika, na unadhani anaweza vipi kikataa milioni kadhaa ambazo vionjo visipotumika hapati hata senti.
Hili bandiko limewekwa kama husda tu kwa Diamond kwani mwenye akili timamu anajua kuwa walishaelewana ki namna flani, hakuna chochote kinachoweza kubadilika kwani hata Akili The Brain si zwazwa na Diamond mjanja hivyo lazima makubaliano yao ni ya kimaandishi.

Swali la kizushi: Wale wenye original song ambayo Akili 'alisampo' wimbo wao na kuchomeka maneno ya Kiswahili aliwalipa?
 
WCB wana legal team, infact kuna mwanasheria wao jina limenitoka. Ni kati ya wasanii wa kibongo wanaozingatia masuala ya kisheria kabla hawajafanya mkataba au kutumia cha mtu. Sina uhakika na wasanii wengine kama kuna chochote huwa wanafanya before kutumia kazi nyingine ya kisanaa, sababu recently kuna nyimbo nyingi sana zimechukua vionjo vya nyimbo nyingine, Msikilize J melody na Mario nyimbo zao nyingi zina vionjo vya kazi za watu wengine, i hope wamezingatia masuala ya kisheria.
 
Nenda kamshauri oyaaaa weee sikia unajuwa anaishi wapi?Anaishi Ilala mtaa wa Songea na Newala karibu na fundi Seti mtengeneza Masubaru.
 
Back
Top Bottom