kagoshima
JF-Expert Member
- Dec 31, 2015
- 2,887
- 5,687
Mie sio mwanasheria Ila iko wazi Luten Urio ni mtu mwenye roho ngumu na ovu sana. Hajawatendea haki wanafunzi wake wa zamani jeshini. Amewatoa hawa watu kwenye shighuli zao binafsi za kujitafutia baada ya kuondolewa jeshini,
Kawadanganya eti kuna kazi ya ulinzi kwa Mbowe kwa maneno yake mwenyewe hapo mahakamani, wakawazungukia kwa nyuma kupitia polisi kuwakamata na kuwabambikia kesi ya ugaidi.
Ndugu Urio kwanini uwaachishe watu kwenye shughuli zao za kujipatia kipato, uwadanganye kuna kazi ambayo haipo halafu mpange na askari polisi kuwakamata?
Nadhani hapo kuna jinai, Afande Urio afukuzwe kazi Jeshini ashitakiwe kwa kosa la udanganyifu na kuleta taharuki nchini.