Nashauri iundwe Tume kuchunguza vifo hivi vya Watanzania wenzetu

Nashauri iundwe Tume kuchunguza vifo hivi vya Watanzania wenzetu

Joined
Jan 30, 2023
Posts
16
Reaction score
14
SIKU za Karibuni kumeibuka wimbi la vifo vya viongozi huku sababu za vifo vyao zikifichwa na mwisho mnawekewa ratiba ya mazishi watu wanatoa hotuba za kusisimua wanaondoka wanaziacha familia kwenye majonzi makubwa hususan watoto na wazazi.

1. Kifo cha KATIBU Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu, Sitta Mashala ayefariki dunia tarehe 11 Novemba 2024 majira ya saa 12.45 jioni katika Hospitali ya wilaya ya Maswa wakati akipatiwa matibabu.

2. Kifo cha Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Christina Kibiki, ameuawa kwa kupigwa risasi kifuani na watu wasiojulikana tarehe 13 Novemba, 2024.

3. Kifo cha Meja Jenerali Mstaafu Charles Mbuge aliyefariki dunia tarehe 12 Oktoba, 2024 alfajiri akiwa Nchi India alipokuwa akipatiwa matibabu.

4. Kifo cha Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Lawrence Mafuru amefariki dunia Jumamosi tarehe 9 Novemba , 2024 katika Hospitali ya Apollo nchini India.

5. Kifo Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile, amefariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 27 Novemba 2024, nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu.

Vifo hivi vina utata mkubwa hasa kutokuwepo na taarifa za viongozi hawa kuugua zaidi ni wananchi kujulishwa wamefariki, lakini nakumbuka wakati wa Jakaya kama kuna kiongozi amelazwa nje ya nchi tuliona picha za viongozi mbalimbali wakienda kuwatembelea wagonjwa huko India.

Kifo cha Jenerali Mbuge nchini India sijui kama wenzangu mliona Picha za Kiongozi wowote wa Jeshi, Balozi au Serikali akienda kumtembelea India, Kifo cha Mafuru nchini India sijui kama kuna picha inayoonyesha kuna kiongozi alikwenda kumsalimia hospitali.

Kifo cha Ndugulile sijaona picha ya Spika wa Bunge, Naibu Spika au Katibu wa Bunge akimsalimia Ndugulile alipokuwa anaumwa India.

Kifo cha Mafuru, sijaoa picha ya kiongozi yoyote wa Serikali akimtembelea Mafuru akiwa anaumwa nchini India

Kifo cha Katibu wa CCM Maswa, sijaona picha ikimuonyesha Mwenyekiti wa Mkoa wa Simiyu akimsalimia hospitali Maswa, wala Katibu wa CCM Mkoa Simiyu, wala Katibu Mwenezi mwenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu...

Hadi leo kwenye kusomwa Wasifu wa Marehemu Ndugulile aliyeandaliwa kusoma ameshindwa hata kuwaeleza watanzania kuwa Ndugulile alikuwa anaumwa nini na alienda lini India kwa matibabu.
 
Back
Top Bottom