Nashauri kabla hujapaka lipstick na lips shine yako nzuri sana, basi safisha kwanza kinywa chako vizuri

Nashauri kabla hujapaka lipstick na lips shine yako nzuri sana, basi safisha kwanza kinywa chako vizuri

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Ni muhimu sana kua karibu na mwenzi wako mkizungumza na kubadilishana mawazo, kwa karibu sana tena kwa kujiamini sana.

Ni muhimu sana muonekano wenu, uwe wa kupendeza na kuvutia ninyi wenyewe na hata kuvutia wengine, lakini ni jambo la maana zaidi, muonekano wenu wa njee uambatane na usafi kamili wa ndani, hususani usafi wa kinywa na kwengineko.

Hii itasaidia kuondokana na uzito wa kuvumilia mazingira magumu ya hewa nzito ya kinywa na maeneo mengine, harufu isiyofaa na kuivumilia, lakini baadhi hujikaza kinafiki kuridhisha wenzi wao, lakini ndani yake ni maumivu makali.

Rangi ya kucha, rangi ya lipstick na mavazi ulovaa, vinaendana na umependeza kweli, lakini hewa inayotoka kinywani chako unapozungumza na watu ni nzito mno, na saa zingine inaakisi kwamba kwenye maeneo mengine huenda ni nzito zaidi.

hata hivyo, usijisahau sana, joto kwa kiasi fulani bado lipo, hasa ukizingatia kazi na na mazingira ya jasho tulonayo. Kung'ag'ana na wigi wiki nzima nayo inazalisha harufu nzito ya uvundo na hivyo kua kero kuanzia ofisini kwa bosi wako, na nyumbani ni mzigo zaidi kwa alekaribu nawe. Anaikinai nyumba yake 🐒
 
Asante kwa kutukumbusha usafi...
Nina Imani na wifi ulimwambia au sio wanawake wenzangu...
 
Asante kwa kutukumbusha usafi...
Nina Imani na wifi ulimwambia au sio wanawake wenzangu...
ni jambo la maana sana hilo hulifanya bila kusahau,
na ni jukumu letu sote, muhimu sana kukumbushana katika hili 🐒
 
Back
Top Bottom