Nashauri Kambi zote za Jeshi zifungwe Camera Maalum na zisilindwe tu physically na Wanajeshi

Wale wanajua wanavolinda kambi zao.
Tuwaamini na tuwaache wao na siri zao
 
Wewe ndiye mpumbavu unayejifanya kujua kila kitu...........
 
Gentamycine naona sasa unaingia anga zingine kabisa issue za jeshi usilinganishe na taasisi zingine kabisa na ndio maana jeshini huwezi sikia vyama vya wafanyakazi.Hii inanipa picha hujapitia jeshi ungepitia usingetoa mawazo kama haya.Swali la wanajeshi kuchunguzana wenyewe kwa wenyewe mbona liko wazi kabisa.Mbona hata sisi wenyewe tunachunguzana wenyewe kwa wenyewe.Kila mwananchi ni mlinzi wa mwananchi mwenzake.Siwezi kuona unafanya maovu mfano unaua na nimekuona kwa macho nikaacha kwenda kukuripoti polisi.Au nione unamtumia mtoto mdogo kingono na ushahidi ninao nikaacha kukupeleka vyombo ya usalama.Kiufupi tu mambo ya usalama wa nchi hasa jeshi hauongelewagi kwenye mitandao ya kijamii
 
Hapa natofautiana na wewe.Huwezi sema wachukuliwe vijana wa division 1 tu.Kumbuka hata wenye elimu za chini wanahitajika sana sema sasa nadhani darasa la saba hawachukuliwi.Elewa vita vinapotokea hakuna cha division wala nini wote ni mstari wa mbele lazima kuwe na wataalamu wachache wa kupiga hesabu za masafa ya mizinga na askari wanaotangulia mbele kwenye mapambano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…