Nashauri kufungwe kamera katika Miundombinu muhimu ili wanaoiharibu walipe faini au waishie jela

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kuna mpuuzi mmoja sasa ni wiki katoka kulewa zake Mbezi Beach Tangi Bovu (jirani na kwa Bujibuji Simba Nyamaume) na akawasha gari yake na kuiendesha spidi na kizembe kabisa akaja kugonga moja ya kingo za Daraja muhimu la Bondeni Kawe na ikabakia kiduchu tu gari lake litumbukie mtoni na tukamuokotee baharini Kawe Beach.

Tayari muonekano wa Daraja hilo muhimu sana umeanza kuwa mbaya kwani kingo mojawapo imepinda huku tena na upande wa pili kuna wapuuzi wengine wawili madereva modaboda waligongana na kuchubua sehemu ya daraja kwa kuwa kote walikuwa wanamuwahi mteja ambaye hata hivyo walimkosa kwani aliwaambia hakuwaita wakamchukue bali kulikuwa ni Kiherehere chao tu cha kutukuka.

Haya wenye mamlaka na miundombinu ya nchi tafadhalini upesi sana nendeni Daraja la Bondeni (shoko) kawe mkalirekebishe kwani kuna moja ya kingo imepinda na inataka kung'oka pia.

Fungeni camera ili iwe rahisi kuwadaka hawa Wahuni na Wapuuzi wanaoiharibu kwa Uzembe wao wa Kulewa na Kuendesha Gari zao kwa Fujo na ama muwalipishe Faini Kubwa au Waamrisheni wakanunue Vifaa walivyoviharibu na wavitengeneze Wenyewe kwa Mikono au Meno yao mpaka irejee katika hali yake ya Kawaida.

Balozi wa Kujiteua Mwenyewe wa Utunzaji wa Miundombinu muhimu ya Tanzania na Mzalendo Mwandamizi GENTAMYCINE nimemaliza.
 
Ajali ikitokea lazima Polisi watakuja ona, sasa kama Polisi hawajawashirilisha TANROADS hapo tatizo no Polisi,vinginevyo TANROADS waweke kikosi kazi
 
Unapoharibu miundombinu inapaswa uwajibike kutengeneza ulichoharibu.

UPO SAHIHI.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Walevi wanapaswa kunyang'anywa leseni na kutaifishwa magari yao, kisha kifungo miaka 45 na viboko 6 kila siku.
Na ikiwezekana wapitiwe na hata kwa Mpalange Kwao ili kuwa Fundisho kwa Wapuuzi wengine wanaofanana nao.
 
Kuna mpuuzi mmoja sasa ni wiki katoka kulewa zake Mbezi Beach Tangi Bovu (jirani na kwa Bujibuji Simba Nyamaume) na akawasha gari yake na kuiendesha spidi na kizembe kabisa akaja kugonga moja ya kingo za Daraja muhimu la Bondeni Kawe na ikabakia kiduchu tu gari lake litumbukie mtoni na tukamuokotee baharini Kawe Beach.

Tayari muonekano wa Daraja hilo muhimu sana umeanza kuwa mbaya kwani kingo mojawapo imepinda huku tena na upande wa pili kuna wapuuzi wengine wawili madereva modaboda waligongana na kuchubua sehemu ya daraja kwa kuwa kote walikuwa wanamuwahi mteja ambaye hata hivyo walimkosa kwani aliwaambia hakuwaita wakamchukue bali kulikuwa ni Kiherehere chao tu cha kutukuka.

Haya wenye mamlaka na miundombinu ya nchi tafadhalini upesi sana nendeni Daraja la Bondeni (shoko) kawe mkalirekebishe kwani kuna moja ya kingo imepinda na inataka kung'oka pia.

Fungeni camera ili iwe rahisi kuwadaka hawa Wahuni na Wapuuzi wanaoiharibu kwa Uzembe wao wa Kulewa na Kuendesha Gari zao kwa Fujo na ama muwalipishe Faini Kubwa au Waamrisheni wakanunue Vifaa walivyoviharibu na wavitengeneze Wenyewe kwa Mikono au Meno yao mpaka irejee katika hali yake ya Kawaida.

Balozi wa Kujiteua Mwenyewe wa Utunzaji wa Miundombinu muhimu ya Tanzania na Mzalendo Mwandamizi GENTAMYCINE nimemaliza.
Dar sio kigali, huku wapuuzi wengi
 
Back
Top Bottom