Genius Man
JF-Expert Member
- Apr 7, 2024
- 1,012
- 2,317
Nashauri kuwe na masomo ya vitendo maalumu kwa jamii pia kwaajili ya kujiandaa na kukabiliana na majanga mbalimbali kama vile moto, mafuriko, matetemeko ya ardhi n.k
kwa mara nyingi masomo ya vitendo vya kukabiliana na majanga pamoja na vifaa vya uokozi huwa vinatolewa kwa asilimia kubwa kwenye vitengo maalumu tu vya uokozi ndani ya nchi, lakini katika uhalisia ni wazi kuwa bado kwa namna moja au nyingine vitengo hivyo havitoshelezi vya kutosha kwenye kufanya uokozi yanapotokea majanga mbalimbali kwenye taifa.
Nashauri kuwe na mafunzo maalumu pia kwa jamii kwaajili ya kukabiliana na majanga hayo tusitegemee vitengo vya uokozi pekee kutoa msaada, jambo hili litasaidia jamii kuweza kujisaidia yenyewe pale inapobidi kujiokoa ili kuepukana na vifo vingi visivyo vya lazima kwenye jamii yanapotokea majanga mbalimbali.
Sambamba na mafunzo hayo ya uokozi kwa jamii nashauri pia kuwepo na vifaa maalumu kwenye maeneo mbalimbali kadri tutakavyoweza kumudu angalau hata kwenye kila ofisi za viongozi wa mitaa kuwe na vifaa hivyo itabidi tukae tuangalie ni vifaa gani tunaweza kuvimudu ili kuisaidia jamii kwenye majanga yanapotokea.
Vifaa hivi pia vya uokozi vinaweza kuwa na msaada mkubwa kwenye upande wa vitengo vya uokozi pale vinapohitajika inakuwa ni rahisi kwa vitengo hivyo vya uokozi kuvipata sio mpaka viende kuvifuata maeneo ya mbali hali inayoweza kuwa na madhara makubwa jamii.
Mwisho, nashauri pia mafunzo hayo yatolewe mashuleni kwa watoto kwa vitendo njia hii naamini inaweza kuwa na msaada mkubwa na kuleta matokeo chanya.