evangelical
JF-Expert Member
- Nov 21, 2011
- 5,035
- 8,218
Habarini,
Nashauri Viongozi wa Chadema kwamba. Kwa kuwa waliruhusiwa kurekodi yote yaliyokuwa yanazungumzwa kwenye kesi hiyo.
(Nimedokezwa na jamaa zangu wa State Attorney kwamba hii ndio iliyowafanya wakimbie kesi kwani uongo wao mwingi uliwekwa hadharani).
Nashauri Uongozi wa Chadema au mtu yeyote aliyefanikiwa kukusanya yale yote yaliyokuwa yanaongelewa Mahakamani kipindi chote cha mashtaka na hadi siku Serikali wanaamua kurusha taulo ulingoni, katika mlolongo wake kuanzia mwanzo aunganishe vizuri kama kitabu au kijarida, in hard copy na soft copy halafu atusambazie hata kwa kuuza.
Mimi binasfi niliweza kusoma baadhi ya mahojiano ya mahakamani hapahapa JF ila sijafanikiwa kuyapata yote. ila nilisoma nyingi siku pata chache siku nilizokuwa busy na safari flani. Aidha kama kuna mtu anazo zote katika soft kopi kwenye mlolongo wa siku kuanzia mwanzo hadi mwisho wake naomba anitumie au anielekeze napoweza kuyapata
Naamini kabisa kwamba Kumbukumbu hiyo itakuwa somo zuri kwa:
Wanafunzi wa Sheria na hata Raia wa kawaida, pia Vionozi wa Polisi wajitafakari kuhusu uweledi wa askari wake, kesi ii imeonyesha umbumbumbu mkubwa sana wa askari Polisi labda nithibitishiwe ilikuwa ni maksudi, yaani askari kabisa anakiri maakamani kwamba haijui PGO, Mawakali watajifunza kupitia Mawakili wenzao akina Malya na wenzake walivyokuwa wanafanya cross examination, kuuliza maswali hadi mtu anaomba po kwamba hajisikii vizuri apelekwe hospitali, Mawakili wa Serikali wajifunze aibu waliyoipata na waone aibu na wakatae kutumika ovyo na wanasiasa waliopo madarakani kubambikia watu kesi hasa wanasiasa wenye mtazamo tofauti na wanasiasa waliofanikiwa kuwa madarakani.
Majaji, jaji aliyeendesha kesi ii amedhalilisha Ujaji ameonyesha ametumika nilifuatilia hoja zake siku ile anaamua kwamba washtakiwa wanakesi ya kujibu nikaona ameshindwa hata kuonyesha kwamba ni vigezo vipi katika ushaidi uliotolewa , alifanya maamuzi ya kiujumla sana, Li Jaji limetoa maamuzi ya hovyo eti washtakiwa wanakesi ya kujibu likaja kuhaibishwa na Nolle prosequi KWA NINI MAJAJI MNAKUBALI KUDHALILISHWA NA Nolle prosequi ZA DPP? Ungesema mapema washtakiwa hawana kesi ya kujibu au mapema tu mnakataa kesi mnamrudisha DPP akajipange upya kama shauri halina credibility majaji myakatae mapema msisubiri mpaka Nolle prosequi.
Kesi hii inaonyesha umuhimu wa katiba mpya itakayotoa uhuru kwa majaji ili waweze kuwa huru kwenye maamuzi, pia katiba itakayo toa uhuru wa Ofisi ya Mwendesha mashtaka mkuu wa Serikali DPP, nilishashuhudia Rais anamuamuru DPP nenda magerezani katoe watu.
Kesi pia imeonyesha matumizi mabovu ya Nolle prosequi, hii sheria ibadilishwe itamkwe wazi Nolle prosequi itakapotumika Serikali ilipe fidia, unakaa na mtu ma miaka halafu unakuja kibuka na Nolle prosequi, kuna mashekhe walikaa ndani miaka 8 Serikali ikaibuka na Nolle prosequi mahakamani.
Hii kesi imekuwa funzo kubwa sana kwetu sote kwamba siku zote uongo na dhulma hazishindi.