Nashauri Prof. Lipumba, Dkt. Slaa, Mbowe, Lissu na Mzee Rungwe wagombee ubunge tu

Nashauri Prof. Lipumba, Dkt. Slaa, Mbowe, Lissu na Mzee Rungwe wagombee ubunge tu

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Kwa hali halisi na mazingira ya sasa ya uelekeo wa upepo wa kisiasa nchini ni dhahiri kwa miaka kumi ijayo, wanawake wana nafasi kubwa mno, hasa kwa nafasi za juu za uongozi wa nchi kisiasa ukilinganisha na wananume wenye sifa kiasi dhidi ya nyingi na za ziada kwa upande wa wananwake Tanzania.

Kwasababu hiyo nashauri viongozi mbalimbali wa kisiasa nchini ikiwa ni pamoja na baadhi yao niliowataja hapo juu, kujikita zaidi kwenye kugombea nafasi za udiwani na ubunge,
ikiwa kweli ni wanasiasa wenye maono na ujuzi wa kusoma majira na alama za nyakati za kisiasa kwa upande wao, na ikiwa kweli wana dhamira ya kusaidia kuchochea maendeleo ya wananchi, Tanzania.

Vinginevyo wakishupaza shingo kwa matarajio hewa, majira, nyakati, uelekeo na upepo wa kisiasa utawanyorosha na kuwapoteza kabisa kwenye medani ya kisiasa kwa aibu na fedheha kubwa bila heshima ambayo wangeipata wakiwa wabunge wastaafu.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
LISSU anampiga Mama asubuhi tu,,hongo za Abduli zimekataliwa😁😆
 
Back
Top Bottom