Nashauri serikali ifute mikopo ya halmashauri badala yake mikopo hiyo ielekezwe kwa wahitimu wa vyuo na walemavu

Nashauri serikali ifute mikopo ya halmashauri badala yake mikopo hiyo ielekezwe kwa wahitimu wa vyuo na walemavu

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari wanabodi..!
Nilikuwa nashauri hii mikopo inayotolewa na halmashauri ifutiliwe mbali badala yake mikopo itolewe kwa wanavyuo wanaohitimu na waliohitimu pamoja na watu wenye ulemavu.

Huu ni ukweli usiopindika mikopo ya halmashauri imekuwa haiinufaishi serikali wala kuwanufaisha wahusika wengi sababu wengi wanaopewa hii mikopo hawana malengo nayo unakuta mtu anapata mkopo anaenda kununu kijora kitu ambacho graduate hawezi fanya kitu kinachopelekea serikali kukosa rejesho la mikopo hiyo.

Lakini endapo mikopo hii itatolewa kwa wahitimu wa mavyuo na watu wenye huitaji mkubwa kama walemavu mikopo hii itakuwa na impact kubwa sana.Pia itapunguza tatizo la ajira nchini na kuwawezesha wahitimu wengi kujiajiri wenyewe .

Kama kuna uwezekano pia serikali iangalie jinsi gani inaweza kuihamishia kitengo kingine mikopo hiyo yaani badala ya kutolewa na halmashauri mikopo hiwe inatolewa na kitengo maarum cha serikali cha uwekezaji ambapo wahitaji watakuwa wanaongezewa maarifa ya uwekezaji kabla ya kupata hiyo mikopo.
 
kwani hao wahitimu saivi hawaruhusiwi kupata huo mkopo?? bro wajiunge vikundi unapata bila shida yoyote mzee
 
Back
Top Bottom