Nashauri serikali isianzishe miradi mipya hadi iliyopoikamilike

Nashauri serikali isianzishe miradi mipya hadi iliyopoikamilike

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
1,108
Reaction score
1,132
Habarini,
Nimetafakari sana na kuona ni vyema serikali ya Tanzania iachane na tabia ya kuibua miradi mipya wakati miradi mingine waliyoianzisha haijakamilika.

Ninachokiona miradi mipya ndiyo cha ufisadi na kukwama kwa miradi endelevu kwa sababu miradi mipya husababisha viongozi kujipatia fedha kwa vikao,10%,nk hivyo fedha zilizotengewa miradi zinaisha kabla ya mradi kuisha na kupelekea viongozi kubuni miradi mipya ili wapige hela.

Kuwe na utaratibu wa kukusanya fedha kwaajili ya miradi ikishapatokana ndiyo miradi ibuniwe kulingana na pesa iliyopo siyo wabunge wanakaa na kipitisha miradi kwa hela itakayo kusanywa ambayo haipo kwamba BAJETI,unapangaje bajeti kwa pesa ambayo hujaishika hapo ndiyo wizi unapoanzia.

Kuna nchi i.e: Bukinafaso ambazo ziliweka utaratibu wa kukusanya fedha kwanza ndipo wanapanga miradi kulingana na fedha iliyokusanywa siyo itakayokusanywa na wamefanikiwa.

Hakuna nchi hasa za Kiafrika zitakazoendelea kwa mfumo wa kupanga bajeti kwa fedha ambayo haipo ni uongo lazima mapato yakusanywe ndiyo bajeti ipangwe.

Kama viongozi wa Afrika hawataacha huu ujinga basi ufisadi na umaskini havitaisha Afrika.
 
Back
Top Bottom