Gudasta
JF-Expert Member
- Jan 25, 2011
- 501
- 788
Kukamilika Kwa bwawa la umeme la Nyerere kumepelekea Taifa kuwa na umeme wa kutosha. Nashauri huu ni wakati muafaka Kwa serikali kupunguza bei ya umeme (token) Ili kupunguza gharama ya maisha na kuchochea shughuli nyingi za uchumi zinazotegemea umeme.
Raisi Samia ana pigia chepuo matumizi ya nishati safi ya kupikia. Natumai bei ya umeme ikipungua watu wengi watapikia umeme na kuacha kutumia mkaa na Kuni. Maeneo mengi vijijini yamefikiwa na mradi wa umeme wa REA, hiyo inaonesha umeme ukipunguzwa bei wananchi wengi waishio mijini na vijijini wataweza kutumia umeme kama nishati ya kupikia na hivyo kuachana na matumizi ya Kuni na mkaa.
Hii itapelekea kuokoa mazingira yetu Kwa ujumla ambayo yanaathirika sana na ukataji miti Kwa ajili ya kupikia.