Nashauri Wizara ya Elimu kufuta utaratibu wa mwanafunzi kufanya mtihani wa Form Four wenye maswali ya kuanzia Form 1 hadi Form 4

Nashauri Wizara ya Elimu kufuta utaratibu wa mwanafunzi kufanya mtihani wa Form Four wenye maswali ya kuanzia Form 1 hadi Form 4

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Wakuu mtakuwa mashahidi, elimu siku hizi duniani imerahisika sana.

Sio vita tena, bali ni kutoana ujinga tu kisha kila mmoja apambane na hali yake akiishafika huko mitaani.

Sasa kumtaka mtu kwa siku moja ajibu maswali ya vitu alivyojifunza kwa miaka minne ni utamaduni uliopitwa na wakati.

Napendekeza tutumie mfumo wa Semister kama vyuoni. Mtu akimaliza kidato amalize na mambo yake.

Form Four kiwepo kipimo cha uelewa tu.

Marekani nchi ambayo ndio role model wa uelewa duniani wanatumia mfumo ninaoupendekeza naamini hata sisi hatujafikia kuwazidi maarifa na ubunifu.

Mawazo yangu ni mazuri, yachukueni au wadau mnasemaje?
 
Kila kitu mnataka urahisi vijana wa siku hizi. Nani kawaroga?

Sasa mtihani ukiwa rahisi na wote mkafaulu kupata daraja A itasaidia nini?

CCM itatawala milele kwa akili hizi!
 
Kila kitu mnataka urahisi vijana wa siku hizi. Nani kawaroga?

Sasa mtihani ukiwa rahisi na wote mkafaulu kupata daraja A itasaidia nini?

CCM itatawala milele kwa akili hizi!
ugumu unafaida gani mkuu?
nadhani tuache tamaduni kuwa kitu kigumu au kinachopatikana kwa mateso ndio Bora.

Kupima uelewa wa 1/1/2020 mwaka 2024 huu ni ugumu wa kujitakia na kukataa kubuni njia bora.

Kwa nini chuo kikuu hakuna Necta au wasomi wa PHD hata wakisoma miaka 10 hawapimwi kwa kipimo chetu o level?
 
Kila kitu mnataka urahisi vijana wa siku hizi. Nani kawaroga?

Sasa mtihani ukiwa rahisi na wote mkafaulu kupata daraja A itasaidia nini?

CCM itatawala milele kwa akili hizi!
Wewe uliposoma mambo magumu umesaidia nini nchi? taifa hili umeliletea nini baada ya kusoma na kufanya mitihani migumu?

Kwani watu wote wakipata A kuna shida gani?
CCM ikitawala milele na ikawa na sera bora na huduma kwa jamii zikapatikana kuna tabu gani? Tatizo sio CCM kutawala, tunataka maisha ya mtu yawe na unafuu kama huduma za kijamii n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hiyo elimu Ngumu ya anayoipenda pia ni mawazo ya CCM anayoipinga.
 
Naungana nawewe mkuu 100%

Ninakila sababu ya kuupinga mfumo unaotumika kwasasa kwanza upo zaidi kwenye kukomoana kuliko kujenga.

Kukariri midude ya miaka minne kwa "o" level ukayajibu siku moja halafu ukayasahau yote uliyokariri kuna faida gani? (shame on you nyote mnaouyetea huu mfumo)

Au kukariri midude ya advance ile kwa miaka miwili yote( kanizaro reaction, projectile, dalton, fluid motion, integration, differentiation, evolution, wave etc) ukayafanyia mtihani kwa siku moja halafu ukasahau faida yake nini (si kujitia inafiki wa nafsi zetu tu)

Ndio maana hawa wanafunzi waliomaliza form4 na six6 hawana cha maana sana mtaani, wakati mwengine bora hata yule aliacha kusoma akiwa darasa la 6..

ELIMU SIO KUKOMOANA WALA KUVIZIANA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ugumu unafaida gani mkuu?
nadhani tuache tamaduni kuwa kitu kigumu au kinachopatikana kwa mateso ndio Bora.

Kupima uelewa wa 1/1/2020 mwaka 2024 huu ni ugumu wa kujitakia na kukataa kubuni njia bora.

Kwa nini chuo kikuu hakuna Necta au wasomi wa PHD hata wakisoma miaka 10 hawapimwi kwa kipimo chetu o level?
Nisaidie kitu. Ugumu ni nini?

Huwezi kuuacha utamaduni unaosema kitu unachokipata kwa kuhangaika huwa bora. Huwezi kupata maisha mazuri bila kuhangaika, kama ambavyo ni vigumu kwa mchimbaji wa almas kuipata kirahisi.

Niambie jambo lolote lililo rahisi kulipata lenye manufaa.

Hapo kwa Necta na PhD nikuache tu. Huna uelewa mpana wa mambo lakini naliheshimu kwa mawazo haya.
 
Wewe uliposoma mambo magumu umesaidia nini nchi? taifa hili umeliletea nini baada ya kusoma na kufanya mitihani migumu?

Kwani watu wote wakipata A kuna shida gani?
CCM ikitawala milele na ikawa na sera bora na huduma kwa jamii zikapatikana kuna tabu gani? Tatizo sio CCM kutawala, tunataka maisha ya mtu yawe na unafuu kama huduma za kijamii n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
Mambo magumu ni yapi?

Hata haya unayojadili ni mambo magumu kupita uwezo wako.

Hunijui. Utajuaje ninesoma mambo magumu?

Taifa hili nimeliletea nini, he unajua sijaliletea taifa hili nini wakati hunijui? Hata haya unayoyaeleza ni mambo mepesi yamekuletea nini wewe na taifa lako zaidi ya kuwa wapiga kura wa CCM na watumwa wa wanasiasa?

Unataka maisha ya mtu yawe na unafuu wakati unapenda social and economic stratification katika jamii yanaleta maendeleo kupitia migawanyo ya watu kwa viwango vya ufaulu?

Oh sorry, hawa ni mambo magumu ambayo hupendi na kamwe huwezi kujadili kwa sababu unapenda mambo mepesi kama ya Wema karudiana na Diamond!
 
La pili wanadhani elimu ni kufaulu, na sio matumizi ya maarifa, na ujuzi katika kurahisisha jambo.

Wanaamini Elimu ni kukaa darasani kwa kipindi chote cha cha muda uliowekwa na kupewa cheti.
Ahsante kwa nyongeza👍
 
Michango yako ni mizuri sana, lakini kwa mazingira ya Afrika tutawapoteza watoto wetu. Kabisa watatoka hawana kitu kichwani. Nchi za wenzetu tayari walishapiga hatua tangia miaka ya zamani, sisi ndio kwanza tunaanza. Mfumo wetu wa elimu ni mzuri ila umekosa practicals and implementation ya yale tuliyo yasoma. Mimi kiukweli masomo yangu niliyo kilemisha nikiwa chuo sijayasahau mpaka Leo, kitu kimoja nilichokosa ni practical za kutosha za hayo masomo. Na kama ningepata practical za kutosha hakika ningefanya mambo makubwa sana Tanzania, ningegundua vitu vingi sana. Ndio maana nikawa nashauri serikali iwekeze kwenye utafiti wa bidhaa za viwandani (research and development) zaidi huko ndiko kutakako iwezesha nchi yetu kuendelea.
 
Kupima uelewa wa 1/1/2020 mwaka 2024 huu ni ugumu wa kujitakia na kukataa kubuni njia bora.

Hiyo tayari miaka 5 mzee baba...hesabu haijawahi muacha mtu salama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ma mbumbumbu utawajua tu kwaiyo unataka mtihani mwepes ili iweje? Nyie ndo mnakuja kuangusha maghorofa na kupasua waatu vichwa badala ya miguu. Asante kwa mada yako mbovu
 
Back
Top Bottom