Nashauri ziwepo fomu maalum zinazotambuliwa na Serikali kwa ajili ya manunuzi wa vitu vidogo

Nashauri ziwepo fomu maalum zinazotambuliwa na Serikali kwa ajili ya manunuzi wa vitu vidogo

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Napendekeza hili kwa sababu nayaona maafa mbalimbali yanayowapata watu kila siku hasa pale wanaponunua vifaa vyao vidogovidogo kutoka kwa watu binafsi kama simu na kadhalka.

Nashauri pawepo na fomu maalum zitakazokuwa zinapatikana katika vituo vya polisi ambazo zitakuwa zikiuzwa kwa shs 5000 na kazi kubwa ya form hizi zitakuwa ni kuthibitisha jina halisi wa muuzaji wa kifaa husika, kitambulisho chake cha uraia alkadhalika upande wa mnunuzi, pakawepo na taadhari juu ya ubaya na madhila ya kununua vifaa visivyo halali na lipi linaweza kutokea na usumbufu wake.
 
Umewaza sana kwakweli, biashara ya used majumbani imeshamiri sana kwa sasa. Katika kipindi cha mpito jitahidi kupata kapicha kamuuzaji, ila bonge la idea.
 
Umewaza sana kwakweli, biashara ya used majumbani imeshamiri sana kwa sasa. Katika kipindi cha mpito jitahidi kupata kapicha kamuuzaji, ila bonge la idea.
Ndio mawazo anayoyataka rais wetu,na litakapo tokea la kutokea hukuwa umejaza form hii uhusishwe na tatizo moja kwa moja tutarahisishia polisi kazi zao.
 
Hii ingefanyika kwa wafanyabiashara wa mafuta ya petroli na dizeli ili kuifuta Taasisi ya linyonyaji ya Ewura ibaki TBS ya taifa.

Atakayeuza mafuta yaliyochakachuliwa alipe fidia ya gari iliyoharibiwa pampu na mfumo wa mafuta.

Hii ya ewura kuchota pesa kwenye kila lita ya mafuta na kuweka mifukoni mwao ni wizi na unyonyaji na dharau kwa tbs na vyombo vya ulinzi na kwa watanzania wanaolipa kodi zao ili tbs walipwe mishahara kwa kudhibiti vitu bandia.
 
Back
Top Bottom