Nashindwa kuelewa 5000/= imebadilika kuwa 1000/=

Am For Real

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2023
Posts
323
Reaction score
770
Wakuu Leo nimeenda kula mgahawa Moja Stendi ya Arusha wali maharage wa 1500 jumlisha soda ya 1000.

Baada ya hapo Mimi na rafiki tukarudishiwa Chenji yeye 2500 baada ya kutoa 5000 na Mimi 7500 baada ya kutoa 10000.

Nilirudishiwa noti Moja ya 5000,noti Moja ya 2000 na shilingi 500 Moja.

Sasa tumezunguka mji sana na huyu rafiki.Na tulipoagana nilikuwa nasikia kitu Sana basi nikasema ngoja nikanunue maji.

Nilinunua maji lakini muda wakutoa 1000 ya kulipa nikakuta nimebakiwa na 3500 mfuko Badala ya 7500

Hii ni kumaanisha noti Moja ya 1000,noti Moja ya 2000 na sh 500 Moja.Nilianza kushangaza hii inakuwaje

Cha kushangaza baada ya kutoa Ile 1000 hela kulipa mtoa huduma anataka anirudishie sh 4000 chenji wakati nimeoka 1000 kununua maji ya sh1000.Basi nikamkatalia.

Nikaingia mfukoni ndipo nikagundua Badala ya 6500 nimebakiwa na 2500.Nikamuuliza yule muhudumu vipi SI umeona nimekupa 1000.Akasema ndiyo sasa nikawa najiuliza 5000 imeenda wapi na hii 1000 niliyotoa imetokea wapi.

Nikaamua kumpigia rafiki yangu tuliyekuwa naye akaniambia na yeye amepoteza sh 1000 na sh 500 nyingine amedondosha chooni.Wakuu hii hali mbona nikitafakari sielewi.

Nashindwa kuelewa kama labda tulikosea kwenda kula ule mgahawa.
 
Wewe sema tu kuwa unahisi umerogwa acha kujifanya huelewi.

Nipe buku nikutumie namba ya Babu Bwazuabwazua wa Lushoto. Ndio anaemtibu February Marope, huyo anatibu kisasa. Una tap tap tu tilktok.
Hela yako yote itarudi na faida juu.
 
Siku hizi kuna chuma ulete za hatar. Unapewa buku unaiona kama elfu 10 na unarudisha chenchi
 
Hujajiuliza kwanini muuza maji alitaka kukurudishia 4000? Maana yake hiyo 5000 haikubadirika kuwa 1000 kama unavyohisi so muuza maji kajipatia 4000 ya bure pole sana.
 
Back
Top Bottom