Nashindwa kulielewa hili gari

Nashindwa kulielewa hili gari

Area 14

Member
Joined
Jun 17, 2022
Posts
53
Reaction score
354
Nimenunua BMW 5 series 2006 kwa mtu ikiwa fresh nimeendesha kama mwezi ilikuwa poa mpaka nilipompa jamaa alikuwa na safari ya Bagamoyo aliporudi nikaichukua kuendesha kidogo nikaona kama nakanyaga sana mafuta gari haiendi.

Nimeenda kwa fundi akasema shida plug nikanunua zikafungwa baada ya kuendesha naona mambo ni yale yale. Nikamuuliza fundi mwingine kasema nibadilishe pump, sijawahi kumiliki BMW before naomba uzoefu wenu wadau kabla sijanunua tena fuel pump.
 
Utanunua vitu mpaka kichwa kikuume.

Usikute ni mafuta tu ya kidebe yamewekwa humo.

Hizo gari zinakuwa sensitive kutrigger trouble codes au kuwasha dashboard lights siyo kama gari za kijapani sijui ni kwanini watu mnakimbilia ramli.

Anza na uliyemuazima gari, kuna nini kilifanyika, aliweka mafuta wapi! n.k.

Ukitoka hapo tafuta mashine ya Diagnosis ufanye diagnosis.
 
Ahsante mkuu nipo ilala nafanya diagnosi nimeambiwa error code P0087 Weak fuel pump

Hiyo ni code ya low fuel pressure kwenye BMW,

Pump inaweza kuwa ni sababu mojawapo, na kuna engine za BMW zina pump zaidi ya moja ile ya kwenye tank na HPFP.

Pia inaweza kuwa Common rail pressure sensor au fuel pressure regulator.

Tafuteni pressure inakopotelea msikimbilie kubadili Pump.
 
Gari inanuka petrol nikoendesha
 
Back
Top Bottom