Nashindwa kumtofautisha Tundu Lissu na Jonas Savimbi

Nashindwa kumtofautisha Tundu Lissu na Jonas Savimbi

digba sowey

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
8,926
Reaction score
17,880
Habari waungwana,Leo tena naomba kuwasilisha hoja ifuatao:-

Katika historia ya ukombozi Wa bara la Afrika katika kujiondoa katika makucha ya Wakoloni na mabeberu waliokuwa wakinyonya bara la. Afrika tunakutana na huyu bwana Jonas Savimbi kutoka Angola.

Kiongozi huyu huyu alikuwa maarufu sana kwa vita vya msituni ambapo habari za kiintelijensia zinadai kuwa Jamaa huyu alikuwa akitumiwa na Mabeberu ili kuvuruga amani na maridhiano ya Taifa la Angola, Mabeberu walimtumia ipasavyo mpaka alipo kuja kuuawa na Jeshi la Serikali la Angola mwaka 2002 kwa kumiminiwa risasi mfululizo na hapo ndio Angola ikapata amani na utulivu.

Kwa Tanzania yetu ya leo tunaye Jonas Savimbi ambaye ni Lissu, bwana huyu amekuwa na nyendo za kutaka kuiingiza nchi katika makucha ya mabeberu kwa manufaa yake, na amekuwa akijiapiza kuwa lazima taifa la Tanzania lisiwe kisiwa cha amani tena, Watanzania wenzangu tuwe makini na akina Jonas Savimbi ambao wanatumika na mabeberu ili kuvuruga amani ya nchi yetu.

Mungu ibariki Tanzania,mbariki Rais wetu pamoja na Viongozi wote wa chama na Serikali

Nawasilisha.
 
Habari waungwana,Leo tena naomba kuwasilisha hoja ifuatao:-

Katika historia ya ukombozi Wa bara la Afrika katika kujiondoa katika makucha ya Wakoloni na mabeberu waliokuwa wakinyonya bara la. Afrika tunakutana na huyu bwana Jonas Savimbi kutoka Angola.

Kiongozi huyu huyu alikuwa maarufu sana kwa vita vya msituni ambapo habari za kiitelijensia zinadai kuwa Jamaa huyu alikuwa akitumiwa na Mabeberu ili kuvuruga amani na maridhiano ya Taifa la Angola,Mabeberu walimtumia ipasavyo mpaka alipo kuja kuuawa na jeshi la serikali la Angola mwaka 2002 kwa kumiminiwa risasi mfululizo na hapo ndio Angola ikapata amani na utulivu.

Kwa Tanzania yetu ya leo tunaye Jonas Savimbi ambaye ni Lissu ,bwana huyu amekuwa na nyendo za kutaka kuiingiza nchi katika makucha ya mabeberu kwa manufaa yake,na amekuwa akijiapiza kuwa lazima taifa la Tanzania lisiwe kisiwa cha amani tena,watanzania wenzangu tuwe makini na akina Jonas Savimbi ambao wanatumika na mabeberu ili kuvuruga amani ya nchi yetu.

Mungu ibariki Tanzania,mbariki rais wetu pamoja na viongizi wote Wa chama na serikali

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndugu unajua hali ya Angola leo?
unaweza kutuambia SAVIMBI na hawa waliopo leo nani ni wanyonyaji ?
 
Nilichokiona hapo ni Savimbi kumiminiwa risasi za kutosha na jeshi la serikali, mengine upuuzi tu, hivi Lissu alianza lini kutimiwa na mabeberu mana kumiminiwa risasi kama Savimbi tyar mlishafanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Tanzania yetu ya leo tunaye Jonas Savimbi ambaye ni Lissu
Ni wazi humfahamu Lissu. Bahati mbaya "naona" unajaribu kutushawishi kuwa ili tupate amani au tusifike huko kubaya basi yamkute Lissu yale yalio mkuta Savimbi. Wamejaribu imeshindikana. Tuombe yasijirudie, anaetaka kupambana na Lissu ajipange tu hadi sasa naona mnatumia zaidi nguvu za dola, vitisho kama unavyoweka wewe na kejeli. Leo kuna mtu anatuambia kuna ugonjwa unaitwa Tundu Lissu ukimsikiliza vizuri unagundua yeye mwenyewe na bosiwe wana dalili zote za ugonjwa huo.
 
Toa hoja Mkuu,je lissu na savimbi hawafanani?

Ninakusikitikia kuwa hadi leo bado umekuwa na moja wa watu wanaotizama upande mmoja wa coin,pata muda au njoo inbox nikuazimishe kitabu kinachoitwa;Jonas Savimbi;A KEY TO AFRICA na Fred Brigland,kisome kwa makini,pia tafuata kitabu kinachoelezea kuhusu hivi vyama vinavyojiita vya ukombozi hasa,Zanu PF,(elewa kundi la Joshua Nkomo kwa makusudi mazima waliitungua passengers aircraft iliyokuwa na watoto wadogo,baada ya kuruka kutoka Victoria Falls),soma pia kuhusu migogoro ya ANC hasa walipokuwa exile na nini kilitokea pale Chunya (Mbeya,Tanzania ),pale Angola kwenye kambi yao,pia soma kuhusu Swapo walivyo deal na wapiganaji wao waliowahisi ni wahaini etcetc,sasa unapokuwa na facts za pande zote mbili inakuweka kwenye position ya kuandika uzi kama huu wa kumlinganisha Mh.Lisu na Mr.Savimbi.
 
Back
Top Bottom