Nashukuru ninachokipata na ninachopewa

Saad30

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2020
Posts
2,737
Reaction score
5,464
Habari wakuu.

Katika huu mchezo wa Maisha Kuna mambo mengi sana Sisi wanaume tunapitia.

Sometimes unaenda kutafuta unarudi na kitu kidogo mfukoni kufika home watoto wanakukimbilia Kwa shangwe Sana. Basi Nguvu ya nafsi inakwambia hawa watoto ndio faraja yako. Unaingia ndani ya nyumba mke naye anatabasamu kuona mume wake umerudi Salama.

Maisha Yana furaha ukiwa karibu na familia yako. Hakikisha hufanyi makosa Yale aliyofanya baba yako.
Mwanaume mwenzangu mpende mkeo na watoto wako mana Hao ndio hujua baba yupo ndani amelala na mama.

Kugombana kupo lakini hakuna jipya chini ya jua Zaidi tunaishi ili tufe.

Salute kwenu brothers ambao mnanipa support pale ninapokwama kiuchumi.
 
Well said bro. Furaha ipo katika vitu vidogo sana tunavyochukulia for granted.

Daima huwa napata faraja fulani nikirudi nyumbani na kukuta shangwe la kupokelewa na watoto, kupewa kesi zao za siku nzima na kukumbishiwa ahadi ya zawadi ulizotoa.

Kwa watoto wetu sisi ni kila kitu kwao. Huwa wanahisi baba anaweza fanya chochote kile, na hiyo inaleta hisia ya thamani kubwa katika mioyo yetu.

Nathamini sana ule usemi wa "chizi akiwa kazini, nyumbani ni baba".
 
Umenikumbusha nilivyokua mdogo, tunafurahia baba akirudi nyumbani na kumkimbilia kumuwaoooo, ilikua best part of our day, I hope kwake naye tulimpa faraja kama watoto.

Familia ni kila kitu 🀍
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…