Nasibu Abdul (Diamond Platnumz) asaini mkataba na kampuni ya muziki ya Afrika Kusini, Warner Music

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610

Msanii Diamond Platnumz, ameandika historia nyingine tena baada ya kutia saini mkataba na kampuni ya muziki ya Afrika Kusini, Warner Music.

Mkataba huo mpya utahakikisha kuwa WCB Wasafi imejumuishwa katika Warner Music Afrika Kusini na Ziiki Media, wakati mtandao wa Warner Music ukisaidia kumfanya Diamond Platnumz na wasanii wa lebo hiyo kupanda hadhira ya ulimwengu.

Diamond Platnumz ni mmoja wa wasanii waliofaulu zaidi Afrika, akiwa ameachia nyimbo zaidi ya 30, ukurasa wake wa YouTube ukiwa na zaidi ya mashabiki milioni tano waliojisajili, na pia ana zaidi ya wafuasi wa Instagram milioni 12.
 
Kwa hiyo tufanye nini sasa? sisi tuko busy na maisha yetu na yeye yuko busy na maisha yake,wewe umetuletea habari zake ili nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…