Kipindi cha Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Dira ya Dunia, kitarusha hewani mahojiano na mshairi-na msanii mkongwe wa muziki wa dansi, Nasibu aka Ras Nas, Ijumaa hii (29 Februari) kati ya saa moja na moja na nusu jioni, au 19:00 19:30 East African Time (EAT).
Mahojiano hayo, yalochanganyika na masala ya vibao vipya toka kwenye nyu albam ya Dar-es-Salaam, yatafanyika baina ya Ras Nas na mtangazaji mahiri wa Idhaa hiyo, Idd Seif.
Baadaye kipindi hicho kinaweza kupatikana kwenye podikasti mtandaoni