Carlos The Jackal
JF-Expert Member
- Feb 6, 2017
- 25,725
- 78,589
Ifike mahali wananchi waache kulialia na kuhitaji kila kitu bure. Hii nchi bado inajitafuta na hata kama tutajipata hatutaweza fikia azma ya kutoa huduma za afya bure.
Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali kadhaa wa kadhaa hasa hizi za wilaya zina kufa kwa sababu ya utoaji wa huduma bure kupita kiasi.
Kwa mfano, hizi pasuaji za wajawazito, unakuta mjamzito anakuja mweupe, na hapo bado anategemea Kila kitu kitolewe bure, kuanzia madawa kabla ya huduma, huduma yenyewe na madawa baada ya huduma, hapo hujaweka vifaa tiba, hujagusia vipimo maabara, nk, kwanini huduma zisishuke? Mnakomaa kutoa huduma, baadae ukimpa prescription arejeshe vyote vilivyotumika Kwa ajili ya matumizi ya hapo baadae, anakuja
mkali, simu mpaka DC.
Pia soma: RC Chalamila asema mjamzito anayegoma kununua gloves akajifungulie nyumbani. Hafai kuendelea kubaki madarakani
Sasa kwa style hii hatuwezi kwenda, ni lazima viongozi wawajibike kqa kusema ukweli na uwazi.
Mbona elimu ni bure, kuna mzazi aliacha kumnunulia mtoto madaftari au kalamu au uniform?
Ni lazima wananchi wajifunze kupewa huduma kwa kushiriki kuichangia, unapoichangia huduma maana yake unatoa mwanya wa kutoa huduma ya dharura kwa mhitaji mwingine hapo baadaye.
Hivi gloves tu ukanunua zako pea 6 ndani ya miezi tisa kwamba nazo zikosekane?
Wanaume tusikwepe majukumu yetu na kutafuta kichaka cha kujifichia kuonekana kwamba tunamtafuta mchawi.
Pia soma: Kauli tata za RC Chalamila kwenye matamko mbalimbali nchini
Mnapeleka wanawake zenu kujifungua Aga khan, Hindu Mandal, mnatoa mamilioni kwa mamilioni, halafu mnakuja kupigia kelele gloves?
Kadi za kliniki za wajawazito siku hizi zinatoka elimu kabisa juu ya maandalizi ya kufanya wakati wa kujifungua nadhani kila Mwananchi awawajibike.
Unapoambiwa jitahidi ubebe kitu fulani na fulan nenda nacho, acha ubishi, kwani nani atakula ma Gloves?
Wanaume wa Dar, wajibikeni mazeee, ACHENi kelele na majungu kwa Rc Chalamila.