George Maige Nhigula Jr.
JF-Expert Member
- Mar 14, 2008
- 470
- 149
Ndugu wana Jamii ya wazalendo,
Ni dhahiri kabisa sera ya majimbo ya chadema yenye lengo la kurejesha mamlaka kwa wananchi, na kuondoa mamlaka ya wateule wachache kama wakuu wa mikoa na wilaya ambao wamekuwa wakiteuliwa kwa kulipana fadhila na kupeana ulaji bila ya kuwa na ridhaa ya wananchi na uwajibikaji wa moja kwa moja kwa wananchi imekuwa tishio kubwa kwa makada wengi wa chama cha mapinduzi. ambao wengi wao wamekuwa wakisubiri na kujipanga kupata ulaji wa chee bila kuwa na uwajibikaji wowote kwa wananchi.
Wimbi tunaloliona kwa viongozi na makada wengi wa ccm kujitokeza na kutumia statement ya Nassari Joshua ambayo ilikuwa poorly phraised! na ambayo mwenyekiti wa chama Taifa Mh. Freeman Mbowe kuitolea ufafanuzi pale pale NMC na kuweka kumbukumbu sawa kuwa huo sio msimamo wa chama. Hii inaonesha kuwa wana ccm wengi wamepata kisingizio cha kuibeza na kuiponda sera ya majimbo ambayo ndiyo njia sahihi ya kuleta uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali zetu vizuri.
Hii sio bahati mbaya kwa makada wa ccm to tie statement ya Nassari(Dogo Janja) Na Sera nzuri ya majimbo, kwani sisi sote tunajua kuwa wana ccm wengi hawaitaki sio kwa sababu ni sera mbaya la hasha! bali inakwenda kuondoa ulaji wa kupeana ukuu wa wilaya na mkoa ambao wengi wamekuwa wakipigana vikumbo kwa kujipendekeza au kufanya kila hila ili wateuliwe.
Hali kadhalika sera ya majimbo itahamisha mamlaka mengi kutoka serikari kuu na kurejesha majimboni ambako watanzania ndio wanaishi, na watanzania wenyewe watapata fursa ya kuwachagua ma governor na leutenant governor, hivyo uwaziri hautakuwa na deal tena na wizara zitabaki kuratibu sera tu! kwa nani hajui kuwa watu wengi wanakimbilia kugombea ubunge ccm ili wawe mawaziri?
Hivyo lazima watanzania tugundue nia ovu ya chama cha mapinduzi kuipiga mbao sera ya ya majimbo kwa mwamvuli wa kuepuka mgawanyiko wa nchi, hicho ni kisingizio ambacho hakina msingi, mbona hivi sasa tuna mikoa zaidi ya 25 na hakuna mgawanyiko sasa tukigawa majimbo ambayo yatakuwa yanajumuisha zaidi ya mikoa mitatu, huo mgawanyiko utatoka wapi?
Ningependa sana kuona makamanda hususani viongozi wakuu wa chama wakaipigania sera hii kwa kutoa elimu kwa umma inayoeleweka, siyo hivi sasa walivyoiacha hewani ina ning'inia bila base na facts za kutosha, la sivyo kwa mwendo huu wa magamba kuposha wananchi wakati wao magamba wanajua fika kuwa SERA YA MAJIMBO ndo mwisho wa ulaji na vyeo vya kupeana.
TUIPIGANIE SERA YA MAJIMBO KWA MAENDELEO YA NCHI YETU, UWAJIBIKAJI NA KUREJESHA MAMLAKA KWA WANANCHI,TUSIKENGEUSHWE NA DOGO JANJA BACKLASH!