We Know Next
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 815
- 381
Ningefurahi sana, na natamani sana kusikia tamko la Mama yetu aliyebeba Bendera ya Tanzania ktk Umoja wa mataifa, Dr Asha Rose Migiro, kuhusiana na uchaguzi unaotukabili wiki chache zijazo. Nasema hivyo kwa sababu kuu 2;
1. Kwa kutumia nafasi yake kama Naibu katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, anayetoka Afrika, tena Tanzania, naamini kabisa anauwezo wa kutoa tamko la Kisiasa kuwaasa watanzania kuhusu uchaguzi huu, kwani nina uhakika kabisa joto hili la kisiasa atakuwa analipata live toka kwa wahabarishaji wake. Nina imani kubwa na tamko lake kuwa linaweza kuwafanya watu wakafikiri kidogo kwa mipango yoyoye ambayo si mizuri inayopangwa kwa uchaguzi huu.
2. Akiwa kama Mtanzania, ambaye anaifahamu vizuri nchi yake, na kwa vile yuko katikati ya watu wa mataifa, lazima atakuwa na wakati mgumu kwa hali inavyoendelea kwa sasa hapa Tanzania. Naamini kuwa akitoa tamko lake binafsi, kama mtanzania, bila kutumia nafasi yake anaweza kabisa kutufanya Watanzania tukafikiria mara mbili, bila kujali tofauti zetu za kiitikadi.
Naamini kuwa uadilifu wake kama Dr Asha Rose Migiro, ndio uliomfikisha pale na wala sio kwamba ni Mwanachama wa Chama fulani.