Nasumbuliwa na homa, mikono na mapaja vinawasha

mkolaj

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2014
Posts
3,023
Reaction score
1,089
Ndugu wanaJF, naombeni msaada wenu kwani najua hapa ndo tegememeo langu kwa hili tatizo. Kiukwel ndugu zangu nimekuwa nikisumbulia na homa ya kuumwa sehemu zote za viungo za mwili wangu pamoja na mwili kuwasha hasa maeneo ya mikononi na mapajani.

Nimeenda hospitalin zaid ya mara 3 kupata tiba ila mpaka leo hii karibu wiki 2 sasa sioni mabadiliko. Jaman ndugu zangu najua humu kuna madaktari bingwa mnaweza kunisaidia hivi dalili nilizozisema hapo kati ni za ugonjwa gani na tiba yake ni ipi?

Tafadhal naombeni msaada wenu hali sio mzuri.....
 
umefanya vipimo vyote pamoja na kile cha angaza?kama bado rudi hospital fanya check ya mwili

 
umefanya vipimo vyote pamoja na kile cha angaza?kama bado rudi hospital fanya check ya mwili
Kiukweli sijafanya vipimo vyote vya mwili isipokua kila nilipokua naenda hospitali na kuwaeleza waganga kuhusu haya maumivi walikua wanachukua dawa na kunipatia kwa kuliona hili tatizo ni lakawaida tu!!! asante kwa ushauri ndugu yangu ZION DAUGHTER
 
TIBA YA MALARIA


Ugonjwa wa malaria umekuwa na tiba za asili nyingi ambazo baadhi tumeshaziandika na zimewasaidia wengi, leo tunawaletea tiba nyingine inayomaliza kabisa maradhi hayo.

Bamia
Chukua mbegu za bamia uzikaange, uzisage mpaka ziwe unga.
Chemsha nusu kikombe cha unga huo katika glasi 2 za maji kisha chuja.

Dozi:
Wakubwa kikombe 1 x 3 kwa siku kila baada ya mlo.
Miaka (7-12 ) anywe nusu kikombe x 3 kwa siku kila baada ya mlo. Huruhusiwi kuchemsha na kuweka bali fanya hivyo kila unapotaka kunywa.
Miaka (2-6) robo kikombe x 3 kwa siku.
Kwa watoto wachanga kijiko kikubwa 1 x 3, mpatie baada ya kunyonya au kunywa maziwa na kushiba.

Papai

Chukua mbegu za papai zikaushe kivulini, baada ya hapo zisage ziwe unga laini.

Dozi:
Weka kijiko kimoja cha chai kwenye uji, kama huwezi kutumia uji unaweza kuweka kwenye chai lakini muhimu sana kwenye uji.
Kwa siku tumia mara tatu.
Kwa mtoto miaka 5-10 unaweza kumgawia nusu ya mtu mzima.
Kwa mtoto wa miaka 3-5 unaweza kumgawia ¼ wote x 3 kutwa.

Alizeti
Chemsha kilo moja ya majani ya alizeti katika lita 2½ za maji kwa dakika 15. Dozi:
Kunywa nusu glasi x 3 kwa siku, tumia tiba hii kwa muda wa siku 5.
Miaka (7-12) ¼ glasi x 3 kwa siku. Miaka (2-6) kijiko 1 x 3 kwa siku.

Kuhusu kuwashwa washwa mikono nenda kapime Hospitali (Allergy) huenda unayo hiyo Allergy

MziziMkavu njoo faster please!
mkuu Arushaone Hujambo lakini? Ukiwa na Swali waweza kunitafuta bonyeza hapa.http://https://www.jamiiforums.com/conversations/add?to=MziziMkavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…