Nasumbuliwa na maumivu ya mguu

Nasumbuliwa na maumivu ya mguu

Melancholic

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2018
Posts
3,076
Reaction score
5,483
Habarini za wakati huu wakuu. Kwanza tumshukuru Mungu kwa kutuamsha salama.
Pili niende moja kwa moja kwenye mada, binafsi huwa nina kawaida ya kufanya mazoezi kila asubuhi ikiwemo joging na mazoezi mengine ya viungo.

Pia huwa ninapenda sana kukimbia mara nyingi huwa natoka kijito nyama mpaka mwenge sometime naenda mpaka lugaro. Sasa mwezi wa nane nikiwa home nilijigonga maeneo ya ugoko kukatokea nundu nikachukulia poa sikupachua wala nini nikawa naendelea kufanya zoezi kama kawaida ila nlikuwa nkitoka zoez naskia maumivu kama ya misuli kuvuta upande ule ule wa mguu nliojigonga halafu kunakuwa na nundu pia maumivu kiasi, nimeendelea hivyo mwisho nikashindwa hata kukimbia nikikimbia basi wiki nzima nakuwa natembea kwa shida.

Nimejaribu kutumia madawa ya kuchua ni kweli yamenisaidia mpaka nikakaa sawa hata kutembea nikawa natembea vzr nilivoona hivo nikajua tayari nimepona basi nimekaa kama wiki nikajiona sasa nipo tayari kuanza zoez kuna siku majira ya jioni nikaamua kukimbia kutoka kijitonyama to mwenge mpaka mlimani city ila wakati narudi nilianza kuhisi maumivu ya misuli inakuwa kama inavuta hivi, bac nimefika maeneo sayansi maumivu yakazidi kuwa makali nikakimbia kwa shida mpaka nikarudi home nikalala maana ilikuwa usiku

Kesho yake nimeamka sikuweza kutembea wiki nzima nikawa nachechemea nikanunua dawa ya kuchua inaitwa Volin nimeitumia wiki mbili nikakaa sawa. Nikawa natembea vzr kabisa tena mwendo mrefu na maumivu yakawa yameisha bac nilivoona hivo jana majira ya jion nimejaribu kukimbia kutoka kijitonyama to makumbusho nimerudi fresh ila leo nimeamka na maumivu makali ya misuli siwez tena kutembea ndugu zangu.

Kama kuna wataalamu humu wa maswala ya afya mnaweza kunisaidia je hili ni tatizo gani na nitumie nini kupata ufumbuzi maana nikitumia madawa ya kuchua nakuwa sawa na kutembea natembea mwendo mrefu tu na sihisi maumivu ila nikijaribu kukimbia bac nakuwa naanzisha ugonjwa upya. Yani siponi moja kwa moja maana nikijaribu kukimbia tu tatzo linajirudia

Mniwie radhi nimewachosha na uzi mrefu ila nimejaribu kuwaelezea kwa kina ili muelewe na niweze kupata msaada maana sasa ni karibia miez mitatu nasumbuliwa na hili tatzo ahsanteni na karibuni.
 
Nenda hospital ndugu usisubiri mpaka moyo uje ukuulize "nisimame mimi au utasimama wewe..?"
 
Back
Top Bottom