Nasumbuliwa na vidonda vya tumbo

Yuas R Sakitwe

New Member
Joined
Jun 12, 2015
Posts
3
Reaction score
4
Habari wana jf, nasumbuliwa na madonda ya tumbo kwa muda mrefu

Nahitaji kujua anayejua herbal clinic ya uhakika (mana wengi dawa sio wa aminifu)

Naomba kuelekezwa herbal clinic inayotoa dawa za uhakika mana nina madonda ta tumbo kwa zaidi ya miaka 10

Shida yangu kubwa imekua TUMBO KUJAA GAS NA KUUNGURUMA licha ya kumeza dawa aina zote za minyoo pharmacy

Hali hyo inanifanya nisiwe na aman kwan kuunguruma kwa tumbo mbele za watu kunikwaza sana sana

Nikiipata iliyoko moshi itapendeza mana kwa muda huu niko moshi japo sio mwenyeji sana.

Naomba kuwasilisha
 
hapo wengine hatutaweza kukusaidia...
 
Mke wangu alikuwa anasumbuka sana na hivyo vidonda vya tumbo.Kuna siku niliingia humu JF nikakuta kuna uzi unaelezea dawa ya vidonda vya tumbo inaitwa mashona nguo.Nikaenda home,nikayachuma mengi na kumchemshia waifu.Alitumia kama wiki hivi.Hajasumbuliwa tena mpaka leo.Jaribu na wewe
 
Mashona nguo ndio majani gani hayo?
 
Sahizi ishakuwa kama dozi yake.Kwa wiki anakunywa mara mbili maji ya mashona nguo yaliyochemshwa.Kikombe cha tobo
 
Ndiyo yale masheri sheri?
 
mashona nguo.Chuma majani yake.Chemsha maji ya vuguvugu na uloweke hayo majani.Baada ya dakika 15-30 chuja hiyo juisi yake unywe robo kikombe.Asubuhi na Jioni
 

Attachments

  • images (3).jpeg
    10.3 KB · Views: 64
  • images (2).jpeg
    37.6 KB · Views: 58
Ingia tu google search hilo jina.Alafu angaliza hizo picha zake.Ni majani flani hivi yanajioteaga tu maporini.Wangoni wanayaita Manyonyori.
wasambaa wanayaita mbwembwe,ni mboga na pia yanatumika kwa ajili ya kuongeza damu kwa wingi na haraka....masoko makubwa pia unaweza kuyapata kama soko la ilala upande wa mboga za majani
 
mashona nguo.Chuma majani yake.Chemsha maji ya vuguvugu na uloweke hayo majani.Baada ya dakika 15-30 chuja hiyo juisi yake unywe robo kikombe.Asubuhi na Jioni
Vipi nikiweka vyote majani,mizizi na matunda nichemshe yote itafanya kazi?
 
Bamia ni wewe tu na uwezo wako wa kuzitumia unaweza,
1. Kuziloweka kwenye maji ya lita 1, zikiwa mbichi baada ya kuzipasua kati kwa dkk 10-15 ukanywa yale maji yake mdogo mdogo siku nzima hadi yanaisha

2. Kuzikata kata vipande vidogo, na kuzichemsha kwa maji vikombe vinne unaweza ukaweka chumvi kiduchu sana au usiweke, chemsha kwa dkk 3-5, zikipoa mimina kwenye kikombe nusu kunywa zote (bamia na maji) dozi ya ×3 kwa siku.... hii kwa lugha nyepesi tunasema mlenda wa bamia na wengi hutumia hii

3. Chukua bamia mbichi na maziwa fresh blend kwa pamoja weka kwenye glass kunywa dozi ya ×2 kwa siku.... hii uwe na roho ngumu kweli kweli ila ukiikazania unapona kabisa ndani ya siku 30 tu

Dozi hizo zote utatumia mfululizo kwa siku 30 kisha utajipima kwa vyakula vinavyokusumbua kama bado utaongeza siku 30 zingine, dawa sio chumvi utumie leo upone hapo hapo wengine tayari vimekua sugu kwa hiyo uponaji wake utachukua muda, pia ukitumia hasa vikiwa vinauma utapata nafuu ya haraka usiache ukajihisi umepona endelea ukamilishe dozi.
 
wasambaa wanayaita mbwembwe,ni mboga na pia yanatumika kwa ajili ya kuongeza damu kwa wingi na haraka....masoko makubwa pia unaweza kuyapata kama soko la ilala upande wa mboga za majani
Vipi huku kusini yanapatiana mkoa gani?
 
wasambaa wanayaita mbwembwe,ni mboga na pia yanatumika kwa ajili ya kuongeza damu kwa wingi na haraka....masoko makubwa pia unaweza kuyapata kama soko la ilala upande wa mboga za majani
mashona nguo ni dawa inayotibu maradhi mengi hata waliopata ajali damu ikawa inavuja kwa ndani ukitumia inatibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…