Elections 2010 Natabiri NEC chini ya jaji Lewis kuvuruga uchaguzi!!

Elections 2010 Natabiri NEC chini ya jaji Lewis kuvuruga uchaguzi!!

Kiby

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2009
Posts
6,921
Reaction score
4,683
Mapingamizi mengi yamefunguliwa na wagombea sehemu mbali mbali.
Wagombea wa ccm walipomtuhumu mgombea wa upinzani kwa kumwekea pingamizi, yule aliyewekewa pingamizi ndie aliyetakiwa kuwakilisha ushahidi dhidi ya shutuma anazotuhumiwa.
Wagombea wa upinzani walipoweka pingamizi kwa mgombea wa ccm, ndio waliotakiwa kuwakilisha ushahidi wa shutuma zao dhidi ya mgombea huyo wa ccm.
Hivyo kwa mwendo huu natabiri uchaguzi kuvurugwa na NEC ya Lewis.
 
Alafu nasikia ata matokeo ya uchaguzi ati tume lazima impelekee raisi kuyaona kabla ya kuyatangaza.

Sipati picha JK akipelekewa kuwa Dr ameshinda naona ataishia kusema badilisha in 2 hrs
 
Binafsi nilidhani baada ya tarehe 19 mwezi huu kila kitu kitaachiwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kumbe Msajili wa Vyama vya Siasa naye bado yumo. Takukuru wamo. UwT na mgonjwa wetu nao wamo. Polisi hawako mbali. Wakurugenzi wa Halmashauri/Miji/Manispaa ndio WASIMAMIZI wa Uchaguzi wa Wabunge. Ili mradi bora liende matokeo yameshaanza kutangazwa!
 
Hivi karatasi za kupiga kura mwaka huu zina muonekano upi?

2005 JK alitangulia katika hizo karatasi Sheria ya NEC inasema MAJINA yawe arrange alpbetically lakina hawakufanya hivyo

Pili, karatasi za kupigia kura zilitengenezwa kwa Technologia ya aina yake mana ukimpigia Pro LIPUMBA ukakunja karatasi ile ALAMA
inaamia Kwa JK
 
Katika jimbo la Mwabara, mgombea wa chadema Daud haruni aliyemwekea pingamizi Lugalo wa ccm, aliambiwa na msimamizi wa uchaguzi kuwa hana ushahidi na au vielelezo vya kutosheleza. Swali hapa ni kwa nini mlalamikaji ndie anaetakiwa kutoa vielekezo vya madai yake badala ya mlalamikiwa kutakiwa kutoa vielekezo vya kuthibitisha anacholalamikiwa sii kweli? kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Masha kudai mpinzani wake kutoka chadema sii raia bila kutoa uthibitisho na badala yake aliyetuhumiwa ndie alietakiwa kutoa ushahidi wa kumthibitisha kwamba yeye raia. Huu ni ukiukaji wa haki sawa ya ushiriki wa masuala yote yanayowahusu raia. Ukiukwaji huu wa haki za msingi unasukumwa na katiba ya nchi kutoruhusu vyombo huru vya kutetea na kusimamia misingi ya ushiriki wa haki sawa, na kukifanya chama kimoja kuwa chama dola dhidi ya vingine. Lazima tuamke na kuukemea huu mfumo kandamizi kabla ya kutuingiza katika machafuko kama ya Kenya. Hakuna asiyefahamu kuwa mauaji ya Kenya yalichangiwa kwa kiasi kikubwa na tume ya uchakuzi katika zoezi lao la kutaka kuchakachua matokeo ya kura za urais.
 
Nisikilizeni Mwanasheria... Anae dai kwamba huyu mtu sio raia, ndo anatakiwa kuleta vielelezo, au kuprove, ikionekana kuna ukweli kwenye madai hayo, basi aliewekewa pingamizi ndo atatakiwa ajibu. na kama mapingamizi ni ya kusema tu kama la Masha, basi msimamizi wa uchaguzi alipaswa kutupilia mbali pingamizi hilo.
kinachoonekana ni mchezo mchafu tu,, wa kutaka kuwaonea wapinzani. Lakini tatizo ni tume huru ya uchaguzi, ndo kitu tunachokikosa TANZANIA.

We need changes "SLAA IS THE CHANGE WE NEED, YES WE CAN"
 
Back
Top Bottom