Umesoma vizuri ulichokiandika kabla ya kupost? Unafuatilia vizuri undani wa vita dhidi ya madawa ya kulevya? Anza na utawala wa Mwl, Mzee ruksa, Mzee wa uwazi na ukweli, vipi kuhusu mzee wa ari mpya nguvu mpya na kasi mpya? Kuna watu wamepoteza maisha yao kwasababu tu ya ufuatiliaji wa biashara ya drugs mkuu.
Siku zote ni vema kufanya tafiti kabla ya kufanya mambo. Kifupi ni kwamba biashara hii inaweza kukomeshwa na kutokomezwa na Mungu pekee sio binadamu kama wewe na mimi. Mifano hai ipo, ukiitaka itafute na kama huamini jitokeze hadharani uone yatakayokupata