Natafuta ajira ya Ualimu (Private School)

Codename96

Member
Joined
Sep 17, 2020
Posts
90
Reaction score
85
Habari za muda huu.

Ndugu zangu mimi natafuta ajira ya ualimu maana maisha hapa Dar es salaam ni magumu sana.

Mimi nilikuja Dar kwa ajili ya chuo tu kwahiyo sina hata ndugu sasa chuo nimemaliza na sina shughuli yoyote.(sikusoma kwa mkopo).

Kijijini kilimo ni cha jembe na hata nauli ya kuendea tu sina. Naishi kwa madeni.

Natarajia kuhitimu degree ya ualimu mwaka huu.

Nina transcript ya matokeo ya semester 5.

Nikipata ajira ya angalau kuniwezesha kulipa kodi na madeni ya gharama za maisha ntashkuru sana.

Ingawa nimetaja Dar es salaam, niko tayari kwenda mkoani ikibidi.

1. Kiwango cha elimu: Natarajia kumaliza BAED mwaka huu hivyo sina cheti, nina transcript ya matokeo ya semester 5.
2. Masomo ya kufundishia: Historia na Kiingereza.

Asanteni. Kama kuna swali lingine ntafurahia kulijibu. Niko tayari kwenda mkoani ikinibidi.
 
Subiri Serikali ikirelease majina, kuna magepu yatapatikana. Pia katika sector ya Elimu mwezi wa kumi na mbili ndio huwa na kazi nyingi.
 
Asante sana ndugu kwa ushauri.

Suala la Application za mwaka huu ni ngumu sana sisi tunaomaliza mwaka huu kupata, kwa sababu hata vyeti vyetu vitachukua muda kutoka.
 
Ndugu zangu tusaidiane. Mji mgumu huu. Niko tayari kufanya kazi hata kwa masaa 12 kwa siku.
 
#Correction: Matokeo ya semester 5 hayana transcript. Hiyo uliyonayo ni provisional results.
Alafu rudi nyumbani kwanza. Hakuna uhusiano wa maisha ya kitaa na degree yako, ukitaka kujitegemea kajipange tena upya hapo ulikuja kwa ajili ya kusoma sio kutafuta maisha.
Tatizo mkijaga mjini mnaishi maisha ya season kias kwamba hata kurudi nyumbani mnaona jau maana mlishanyea kambi.
Nasisitiza rudi kwenu kwanza.
 
Mkuu omba kazi ya ulinzi

Kwa mwezi 250k unachukua bila wasi wasi

Nenda mikochen wanachukua hadi sasa

Unafanya kazi saa 12 tu unatulia

Kana upo tayar, fuatilia ndan ya Wiki tatu utakuwa umeshapata kazi, bila hata kuwa na connection wala nini
Ni juhudi zako tu
 
Ofisi yao iyo Gardaword ndio pale Mikocheni Warioba ukitokea Scott Pizza.
 
#Correction: Matokeo ya semester 5 hayana transcript. Hiyo uliyonayo ni provisional results.
Alafu rudi nyumbani kwanza. Hakuna uhusiano wa maisha ya kitaa na degree yako, ukitaka kujitegemea kajipange tena upya hapo ulikuja kwa ajili ya kusoma sio kutafuta maisha.
Tatizo mkijaga mjini mnaishi maisha ya season kias kwamba hata kurudi nyumbani mnaona jau maana mlishanyea kambi.
Nasisitiza rudi kwenu kwanza.
Acha upotoshaji wewe.
 
Habari za muda huu.

Ndugu zangu mimi natafuta ajira ya ualimu maana maisha hapa Dar es salaam ni magumu sana.

Mimi nilikuja Dar kwa ajili ya chuo tu kwahiyo sina hata ndugu sasa chuo nimemaliza na sina shughuli yoyote.(sikusoma kwa mkopo).

Kijijini kilimo ni cha jembe na hata nauli ya kuendea tu sina. Naishi kwa madeni.

Natarajia kuhitimu degree ya ualimu mwaka huu.

Nina transcript ya matokeo ya semester 5.

Nikipata ajira ya angalau kuniwezesha kulipa kodi na madeni ya gharama za maisha ntashkuru sana.

Ingawa nimetaja Dar es salaam, niko tayari kwenda mkoani ikibidi.

1. Kiwango cha elimu: Natarajia kumaliza BAED mwaka huu hivyo sina cheti, nina transcript ya matokeo ya semester 5.
2. Masomo ya kufundishia: Historia na Kiingereza.

Asanteni. Kama kuna swali lingine ntafurahia kulijibu. Niko tayari kwenda mkoani ikinibidi.
Ajira katika shule binafsi kwa kiwango kikubwa zinapatikana Dar es salaam, usijaribu kutakaka kurudi kijijini kama kweli unahitaji ajira

Chakufanya kwa wakati huu kuwa tayari kwa kujitolea kwa zaidi ya miezi sita kufundisha bure katika shule yoyote ile ya private, primary au secondary ili uweze kuwa na uzoefu

Baada ya hapo utapata connection na kazi bila nguvu kubwa
 
Back
Top Bottom