Natafuta biashara ya kufanya ya mtaji wa Mil 5

Deryck Leon

New Member
Joined
Jan 4, 2017
Posts
4
Reaction score
4
Jamani salama umu ndani,

Ebhna mi nina milioni 5 zangu, natafuta biashara ya kufanya ili niweze kuizalisha hii pesa iingie kwenye mzunguko.

So natafuta wazo la biashara ambalo linaweza kuwa zuri, kuendana na huu mtaji. Nipo Dar es Salaam wakubwa.
 
1. Tafuta frem sehemu iliyochangamka fungua goli la vinywaji. Hapo unaweza Anza na mili 3.

2. Fungua library ya kubani muziki huo mtaji unafit kabisa kufungua ofisi nzuri kwa siku 15-20 haikupigi chenga pia unaweza ongezea biashara nyingine Kama kuchaji simu na vinywaji

3. Tafuta site yenye mkusanyiko wa watu anzisha kijiwe kisafi Cha supu chapati na maandazi....
Chagua hapo
 
Una roho ngumu na umeaga kwenu?.
=Kama jibu ni ndio

Kafungue ofisi ya mikopo ya kausha damu hapo dsm, majinga mengi sana utakula hela zao sana

[emoji3] Ukizichekea pisi za uswahilini zitamaliza mtaji huo.

[emoji3] Kama una roho ya huruma achana nayo io ishu.

[emoji3] Kuhusu vibali na gharama zake sijajua maana sio mzoefu ila nimeshuhudia mshikaji wangu ameajiliwa kwenye ofisi hizo pesa wanazikusanya tu.

[emoji3] Kuna wadaiwa wasumbufu jiandae.

[emoji3] Mtaji kianzio million tatu tu inatosha io nyingine utaiweka kama tahadhari na kukuzia mtaji.

[emoji3] Mjumbe, sijui mwenyekiti au balozi jenga nao mahusiano mazuri pia usiwasahau katika moja na mbili (buku mbili mbili za soda).

[emoji3] Kua makini na pisi kali

[emoji3] Kua makini na pisi kali

[emoji3] Hawa jamaa wenye hizi ofisi wanapiga pesa aisee na watu wanashida na hela mtaani lazima waje tu.

[emoji3] Sema kama utaifanya hii ishu badili mfumo tofauti na wafanyavyo wengine usitake faida kubwa kama wengine cheza na akili za wateja wako ionekane unawapa unafuu ila kiuhalisia unawapiga, weka riba ya 20% pia rejesho lianze kurejeshwa baada ya siku saba kuhusu faini hilo utajua wewe uweke ngapi ila buku kwa siku inatosha wengine wanafanya buku mbili.

[emoji3] Kwanini riba iwe 20% na rejesho lianze baada ya wiki tofauti na wengine wafanyavyo (riba 30% na rejesho siku moja baada). Usitake mafanikio ya haraka we inuka mdogo mdogo pia utavutia wateja wengi.

[emoji3] Narudia tena changamoto kuu ni pisi kali usipokua makini tu zinakufilisi

[emoji3] Vitu wanavyoweka dhamana hakikisha vina uhalali.

NB. Sina uzoefu na hii biashara na sijwahi ifanya nimekaa kwenye hizo ofisi mara kadhaa nilipokua naenda kumtembelea mshikaji kwahiyo kama utapendezwa nayo fanya utafiti mwenyewe nachokuhakikishia tu ukipata mzunguko mzuri pesa ipo.
 
Kama unataka ajute ajichanganye hapo....
Na uzoefu mkubwa Sana na hiyo biashara Tena kwa Dar ndo asijaribu kabisa kwanza tu huo mtaji n mdogo Sana....
Hiyo biashara walau uwe na mil 15... Tena kwa wiki ndo atoboi kabisa Bora hata kwa siku [emoji2][emoji2][emoji2]
Faida ya kwa siku iko hivi wakileta Leo hela ndo hizohizo utakazo kopesha Sasa wiki sijui Kama utatoboa...
Mfano kwa siku wakija kukopa wateja 18 wa laki 3 unatakiwa uwe na mtaji walau mil 6..... Bora kwa siku unaweza wabalance otherwise uifanye in local way
 
Kwakua ndio ana anza M 15 mbona ndefu sana mimi nimemshauri hivyo maana anahitajika kuanza pole pole kabla hajakuza mtaji na kupata uzoefu, mimi io ofisi nayoisemea walianza na M 5 tu ila sasa wanasema inafika 18M na hata miezi 6 hawaajatimiza labda kama wamenificha.
 
Hao n waongo mfano hizo ofisi unazoona haziko hivo Zina chain ndefu wanaanza leo na mil 5 wanaweza kuzigawa Leo zikaisha halafu wakaongezewa hela na maboss wao....
We fikilia wateja 30 utawapa kweli hiyo 5??? Kwa mwezi mmoja tu Tena kwa ofisi mpya unaweza kugawa Hadi mil 40
 
Ka Ma upo serious vile kumbe aaah wapi
 
Inawezekana na kuna kama mara mbili niliona wanafunga ofisi na mtunzaji wao pesa aliondoka na 1.5M na mara ya pili 2.4M ambazo ni nje na walizokopesha io siku.
 
Chagua hapa kama ujaridhika nikuongezee orodha
IDEAS ZA KUTOKA KIMAISHA KWA MTAJI MDOGO


1.Nunua pikipiki ya Dhamana ukaanza biashara ya Boda boda.
2.Fungua saluni
3.Mradi wa tofali za kuchoma
3.Fuga kuku
4.Somea ujuzi wowote
5.Mradi wa kushona nguo
6.kijiwe cha kuchomelea
7.kijiwe cha milango na madirisha ya aluminum
8.Mgahawa Mdogo
9.Kijjwe cha kahawa
10.Mashine ya kupukuchua mazao mfano mahindi, mpunga, mtama, karanga, nk
11.Mashine ya kukata nyasi, kupalilia
12.Kuuza mbuzi, kuku,
13.Biashara ya mazao.
14.kukodi bus, daladala na kuzisimamia upate cha juu
15.Kutengeneza sabuni, sanitizer, handwash,
16.Kutengeneza unga wa lishe
17.Kilimo cha umwagailiaji water pump, mbegu, madawa
18.Jiko la supu
19.kutengeneza mkaa mbadala
20.Kuuza chips
21.Kukaanga kuku
22.Kutengeneza vitafunio
23.Kuzalisha ethanol
24.kufuga poko mbuzi katoliki
25.Kufungua kilabu cha pombe za kienyeji
26.Kufungua vijiwe vya Kukusanya ubuyu maporini yakitimia magunia unaleta mjini
27.Kuuza juice
28.Kuuza juice ya miwa
29.Kijiwe cha kukaanga samaki jioni
30.Shughuli za upambaji kumbi
31.Kusambaza bidhaa majumbani
32.Kusambaza bidhaa basic needs kwenye maduka ya vijijini yaani unanua mjini unasambaza kwa oda viduka vya vijijini.
33.Kuzunguka minadani kuuza nguo za mitumba, vyombo, nk
34.Kufungua tuition center
35.Kufungua grocery
36.Kuwa wakala wa bidhaa za viwandani
37.kijiwe cha kukusanya taka za plastic, chuma,oil chafu na tairi chakavu.
38.Kufungua genge la kuuza basic home need
39.Kufungua ofisi ya kupiga nguo pasi.
40.Ofisi ya kutengeneza viatu na mabegi
41.Kutengeneza vyombo vya kupikia mfano, majiko, ndoo, sufuria, mifuniko, vikaangio, nk
42.Saluni ya kutengeneza kucha za wanawake
43......Jengea vyumba vitatu wazazi wako nyumba ya Bati upate baraka
44..Nunua shamba
45.Nunua ng'ombe wadogo watano kwa laki na nusu anza ufugaji.
Au nunua mbuzi anza kufuga
46.Fungua kijiwe cha kuonyesha mpira
47.duka la nguo za kupoint classic za mitumba piga pasi tundika kwenye enga
48..Ofisi za baiskeli za kukodi hapo unapata baiskeli nane
49..Duka la spea za pikipiki na baiskeli
50.Duka la dawa na vipodozi
51..ofisi ya kuchaji simu kwa sola vijijini
52..ofisi ya uwakala wa kutuma na kutoa pesa
53.. Bustani za kuzalisha miche ya miti na matunda
54... Ufugaji nyuki na kuuza asali
55.. Kuzalisha unga wa muhogo
56..Direct sale yaani door to door delivery hapa unakuwa na torori na speaker unapita KILA nyumba unauza bidhaa na kuchukua oda ya nini wanataka Ili kesho uwaletee.
57.Utengenezaji pellets chakula cha mifugo,samaki.
58..unga wa lishe
59..mikeka
60.bidhaa za mianzi.
61.utengenezaji wine,
62.usafi wa majumbani
63.kuuza uji wa ulezi,mchele
64.utengenezaji mbolea za mboji na za maji.
65.utengenezaji wa vigae vya cement na vya udongo.
66.kupanda miti kwa ajili ya nguzo na mirunda
67.utengenezaji wa ndala
68.utengenezaji viatu
69.Upondaji kokoto
70.ufundi simu na radio
71.Utengenezaji mifagio
72.utengenezaji crips za Mihogo,ndizi,viazi,nk
73.Utengenezaji tambi,ubuyu
74.panda mlonge,au nyonyo,au mibono au muarobaini Ili uje uuze mafuta,au utengeneze sabuni.
75.Kutengeneza siagi ya karanga
76.Home delivery hapa ni kupita KILA nyumba na kuchukua oda za mahitaji yao then unaenda kununua unawaletea
77.Utengezaji wa vifungashio vya karatasi
78.utengenezaji mitungi,vyungu,majiko ya udongo
79.Kuwatengeneza kucha wadada
 
We unafanya ipi kati ya hizo?
 
Inawezekana na kuna kama mara mbili niliona wanafunga ofisi na mtunzaji wao pesa aliondoka na 1.5M na mara ya pili 2.4M ambazo ni nje na walizokopesha io siku.
Hahhahahaha hapo uwezi elewa hizo fedha anazotunza zina ufafanuzi yaani hapo Kuna zile za fine na zingine siwezi kukuelewsha kirahisi Ila jua mambo hayako Kama unavoyaona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…