Habari wana JF,
Mimi ni software engineer mwenye uzoefu, na nina ham kubwa ya kuingia kwenye ujasiriamali wa kiteknolojia – hususan kutengeneza mifumo inayotatua changamoto kwenye jamii yetu.
Miezi michache iliyopita nilisafiri kwa mara ya kwanza kwa kutumia
SGR, na kwa kweli experience ilikuwa nzuri sana. Nawapongeza TRC na serikali kwa hatua hiyo kubwa.
Lakini wakati wa kutumia
mfumo wa ukataji wa tiketi mtandaoni, niliona changamoto kadhaa – mfano:
- Kuchelewa kwa OTP au kutopokelewa kabisa
- Kukosekana kwa mobile app rahisi
- Mfumo kuwa mgumu kutumia kwa mtu wa kawaida
Hali hii ilinipa motisha ya kuwaza kutengeneza
suluhisho mbadala,
Mpaka sasa tayari nimeanza ujenzi wa mfumo wa software unaoweza:
- kuruhusu abiria kukata ticket kwa urahisi kupitia (mobile apps)
- kufuatilia ratiba za treni
- Kutoa taarifa za vituo, bei, na nafasi zilizobaki
- online payments integrations (banks, mobile Money + azam pesa)
- Ku-support auto ticket printing
- Kuwa na offline access kwa tiketi
- Customer care dashboard
- Advanced dashboard kwa TRC
🔍 Kwa Nini Nimeamua Kuanza Huu Mradi?
Kabla ya kuanza ku-code nilifanya research kidogo kuhusu mfumo unaotumika sasa, kwa sasa TRC wanatumia mfumo uliotengenezwa na
EGA (e-Government Authority), ambao hutengeneza mifumo kwa taasisi za serikali. Mifumo hii ni mizuri sana kwa matumizi ya ndani ya serikali (internal government use), kama hospitali au wizara, ambapo wananchi wanasaidiwa na watumishi wa serikali kutumia mfumo.
However, for services like train booking where the end users (ordinary people) need to interact directly with the system using their phones, we need something more modern, simpler, and mobile-first
🧩 Mfano mwingine halisi:
Shirika la ndege
Air Tanzania (ATCL) lina partnerships na makampuni binafsi ya teknolojia kwa ajili ya mfumo wao wa tiketi na operations. Hii inaonesha kuwa
TRC pia inaweza kushirikiana na innovators kama sisi, ili kuleta mfumo bora zaidi.
💼
Mfumo wa mapato (Revenue Model):
Tutakuwa tunakata
asilimia ndogo kwa kila tiketi inayokatwa kupitia mfumo wetu
Ninachotafuta kwa sasa:
Natafuta
Co-Founder ambaye ana:
- Ana passion ya kutatua changamoto kwa kutumia teknolojia
- Uwezo wa kushughulikia upande wa Business Development, Strategy, na ikiwezekana connections serikalini / TRC
Ikiwa unaamini unaweza kuleta impact kwenye sekta hii, tuma DM au tuwasiliane kupitia email/WhatsApp (nitatoa kwenye inbox).