Nimeona umeanzisha thread nyingi zinazofana na hii.
Nakumbuka ulileta thread hapa unatafuta tiba ya depression na wadau walijaribu kukushauri kadiri ya upeo wao.
Swali kwako. Je, ulifanyia kazi ushauri uliotolewa?
Kwauzoefu wangu watu wanaopitia matatizo ya msongo wa mawazo huwa wanashindwa kufuata ushauri wanaopewa kwa makini.
Anajaribu hili siku chache asipoona matokea anarukia jambo jingine. Na inakuwa hivyo siku zote.
Nimesoma baadhi ya thread zako na nimegundua kitu.
Wewe huna chanzo kizuri cha kukuingizia mapato na hiyo inasumbua akili yako kupelekea over thinking.
Tiba muhimu kwako si ganja au aina yoyote ya pills.
Jitahidi kutafuta kazi uwe na kipato.
Pia kama huna mwenza tafuta itasaidia kupunguza mawazo.
Mahusiano ni muhimu hasa kwa watu wanaopitia hali kama yako.