Natafuta gereji ya malori, lengo kuu ni kujifunza kitengeneza na kutimiza ndoto ya kuwa dereva wa lori.

Natafuta gereji ya malori, lengo kuu ni kujifunza kitengeneza na kutimiza ndoto ya kuwa dereva wa lori.

Joined
Aug 10, 2022
Posts
45
Reaction score
53
Habari ndugu wa jukwaa hili na wanajf kwa ujumla..

mimi ni kijana miaka 24 kabila msukuma naishi tabora, nina elimu ya kidato cha nne. Niko hapa kuomba sehemu ya kufanya kazi (Gereji) kama nilivyotaja hapo juu.. pia ikiwa ni pamoja na kupata konection na madereva wa malori maana ndoto yangu ni kuwa dereva

mimi ni mtu mwaminifu mwenye hofu ya Mungu, mchapa kazi na situmii kilevi cha aina yeyote, hivyo ninaomba sana kama kuna mtu anagereji yake/yao aweze kunisaidia ili nami niweze kufanikiwa ndoto zang. Lakini pia kama kuna mtu anahitaji kuwa na mtu wa kushoto kwa madereva wa transit nipo tayari kufanya kazi kwa uaminifu mkubwa sana.

Ndoto yangu hii kuifikia naihitaji watu hata kama mm sitakua na cha kuwalipa lakini Bwana atawalipeni kwa wema wenu.

Sina mengi ya kusema zaidi ya kuwakaribisha hapa uzini au PM kama utahitaji maelezo zaidi yanayonihusu mimi binafsi.
 
Back
Top Bottom