Natafuta Hostel ya bei nafuu Dar

Natafuta Hostel ya bei nafuu Dar

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
8,273
Reaction score
13,567
Wakuu habari zenu?

Nina kijana wangu wa kiume anataka kuja DAR kuanza kazi hivyo anahitaji kupata malazi/accommodation ya bei nafuu wakati akijipanga kutafuta chumba na vitu vyake.

Kazi yake ipo maeneo ya Posta hivyo anatafuta malazi yaliyo jirani na hapo au angalau apande daladala moja wakati wa kwenda na moja wakati wa kurudi Posta.

Asanteni.
 
Kwa njia ya kwenda posta atafute sehem za mwendokasi tu, japo hostel wamiliki hua wanataka wanafunzi sana. Ni bora ajichange tu asogee zake maeneo ya Tiptop Manzese hapo anaeza pata chumba hata kwa 60k kizuri tu na usafiri wa mwendokasi uhakika yani.

Au urahisi zaidi ni kama atakaa Kigamboni, japo kule usafiri wa ferry sio wa kutegemea sana.

Ungewahi mapema kuandika hii ningeweza kumuachia ninapokaa pakamsogeza, kuna mtu tayari sahivi.
 
Wakuu habari zenu?

Nina kijana wangu wa kiume anataka kuja DAR kuanza kazi hivyo anahitaji kupata malazi/accommodation ya bei nafuu wakati akijipanga kutafuta chumba na vitu vyake.

Kazi yake ipo maeneo ya Posta hivyo anatafuta malazi yaliyo jirani na hapo au angalau apande daladala moja wakati wa kwenda na moja wakati wa kurudi Posta.

Asanteni.
anakuja lini nije nimstiri?
 
Kwa Posta changamoto, akae mahali strategically ambapo atapata mwendokasi moja kufika karibu then atembee.

Mahali popote kuanzia Mbezi ya Kimara karibu na Morogoro road to Kinondoni. Mimi nashauri atafute mahali ya kufikia one week then mwache apambane mwenyewe.
 
Pale sinza mugabe Kuna royal court ni nzuri San pia atafute chumba maeneo ya kimara hakozi
 
Back
Top Bottom