Natafuta karanga/ndizi

Black Mann

Senior Member
Joined
Jun 30, 2020
Posts
140
Reaction score
209
Habari ndugu zangu,

Naomba kwa anayejua mkoa naoweza kupata karanga nzuri zile kubwa kubwa kidogo, sio hizi ndogo ndogo (wakulima / wauzaji wanajua)

Pia, naomba kwa mtu anayeweza kujua zinakopatikana ndizi za kuiva zile ndogo ndogo.

Karanga nataka zije Dar!! naombeni bei elekezi kwa kilo.
 
Ndizi Arusha bei inaanza 7000 mkungu
 
Karanga Wahi Mbeya, Dodoma, Tabora
 


Karanga na ndizi za uhalisia au za tafsida???.

Mfano unaposema "Nzi wa kijani" kwa tafsida inajulikana ni Chama fulani kikongwe cha siasa.
 
Hasara za kukomenti usingizini hizi.

Jibu lilikuwa litoke kwa mleta mada kwamba; ni karanga na ndizi halisi.

Wewe hujasikia akina dada wakisema; hawajazoea wao ni sungura hawajazoea maharage wamezoea karoti.--- hiyo ni tafsida.

Nenda kajifunze lugha.
 
Jibu lilikuwa litoke kwa mleta mada kwamba; ni karanga na ndizi halisi.


Wewe hujasikia akina dada wakisema; hawajazoea wao ni sungura hawajazoea maharage wamezoea karoti.--- hiyo ni tafsida.

Nenda kajifunze lugha.
Kwan hauwezi kusoma hata uzi upo jukwaa lipi? Nshafahamu sasa kumbe una shida mahali,nilijua ni maruweruwe ya usingizi kumbe sio.
 
Karanga za aina hiyo nenda Tabora na eneo la Inyonga wilaya ya Mlele utakusanya mpaka utapike

Za maganda kilo @ 400/= na ukimenya debe linatoa kilo 7
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…