Kama una Bachelor, wewe tayari ni mtaji hutakiwi kupanic wala kwenda papara papara. Tulia, jipange vizuri, angalia opportunities ziko kibao. Mashule mbona yako mengi hayana walimu, mbona inshu zipo nyingi sana sema una wiki kama 2 ~ 3 tangu umalize shule ndo kwanza umeingia kwenye soko la ajira.
Acha kuwa na wasiwasi, najua wakati mwingine unalala njaa, lakini usihofu ni mpito huo, wakati mwingine unakosa hela ya vocha au nauli kutokana na background za maisha kuwa tofauti hilo lisikupe stress, na unatamani sana uachane na mambo ya kuingia home saa 12 jioni ka kuku lakini yote hayo yanatokea kwa sababu huenda inakupasa ipitie hao ili uone/ujifunze kitu.
Ushauri wangu: Tafuta pa kuanzia, pawe pana mshahara mdogo we anza nao huku ukijipanga! naimani hiyo bachelor umeipata kwa kujifunza vitu vingi vinavyoweza kukabiliana na hali yeyote ile, so don't worry brother/sister just relax and increase your concentration in your job hunting.
Utakuja kupata kazi na utasahau JF mpaka tutakapokubandika hapa jamvini umefisadi sehemu ndo utarudi (just kidding anyway). Good luck!!