Try the USA
Huko nako kama hujasomea elimu yako huko kupata kazi ni ngumu nasikia, Wanaona elimu toka taifa lingine hasa Africa kama siyo bora kama ya kwao. Mpaka waone kuna kitu kinafanana na cha kwao ndo wanaweza kukufikilia. Isitoshe wengine huko nasikia nchi kama Tanzania hawaijui ndo Umwambie umesomea degree yako tz wala hakufikilii hata kidogo. Kaa hapa hapa bongo. Kuna rafiki yangu alishawahi kunambia baadhi yao walikuwa wanajua Africa ni nchi nayo, inasikitisha lakini kutojuwa jeografia japo kwa upande mwingine siwarahumu maana wanajiona wao ndo super power hawahangaiki kujuwa duniniani huko kuna nini. Wanazijuwa tu nchi wanazopigana nao Ugaidi na baadhi ya nchi chache za Africa zenye matukio.