Jamani muwe na staha kidogo hiki kipindi ni kigumu sana, vyuo kibao vimetema, UDSM, MZUMBE, IFM, etc. watu wanataka kazi kweli hasa ukizingatia kuwa ameandika jina lake halisi (Not sure lakini). Mkuu Thabiti najua umejiunga hapa mahususi kwa lengo la kutafuta kazi, na huenda hata pesa ya kuingilia internet cafe ikawa mgogoro, ila usichoke usikate tamaa, andaa CV yako vizuri ili uweze kuvutia interest ya waajiri. Usiwe too general ACCOUNTANT una CPA?, B.Com Acc?, BAF?, Adv Dip in Acc?, Atec 1 or 2?. Fanyia kazi haya mambo utapata kazi tu.